October 29, 2020

 


KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck raia wa Ubelgiji, ameonekana kuteseka kwa dakika 270 ambazo ni sawa na mechi tatu mbele ya kocha mzawa, Charles Boniface Mkwasa.


Sven na Mkwasa wamekutana mara nne katika michuano yote na Mkwasa kuonekana kufanya vizuri katika mechi tatu ambapo ameshinda mbili na sare moja, huku akipoteza moja mbele ya Mbelgiji huyo.

Mkwasa ambaye kwa sasa ni kocha mkuu wa kikosi cha Ruvu Shooting, alianza kukutana na Sven Januari 4, mwaka huu katika mechi ya Ligi Kuu Bara iliyomalizika kwa sare ya 2-2.

Katika mchezo huo, Mkwasa ndiye aliyekuwa kocha anayekinoa kikosi cha Yanga ambapo alipindua meza kibabe kutoka 2-0 hadi 2-2 dhidi ya Simba.

Machi 8, mwaka huu, Mkwasa akiwa kocha msaidizi wa Yanga, timu yake ilishinda 1-0 dhidi ya Simba ya Sven katika Ligi Kuu Bara.

Julai 12, mwaka huu, Simba ya Sven iliichapa Yanga mabao 4-1 katika nusu fainali ya Kombe la FA. Hapa Mkwasa alikuwa kocha msaidizi wa Yanga.

Oktoba 26, ilishuhudiwa Mkwasa akiliongoza jeshi la Ruvu Shooting, alishinda 1-0 katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Uhuru jijini Dar.

Mechi tatu za kwanza, wawili hao walipambana Uwanja wa Mkapa jijini Dar na Sven alioja joto ya jiwe.

3 COMMENTS:

  1. Mie huwa nashangaa tatizo la klabu kubwa Yanga,Simba na Azam kukimbilia makocha wa kigeni na unakuta hawana mapya zaidi ya makocha wetu wazawa na wanapata shida sana kuzifunga hizi timu zetu tunazoita ni ndogo.Ushindi ni wa bahati au unapatikana Kwa mbinde.Kocha Kibaden akishirikiana na kocha muethiopia kama msaidizi wake waliifikisha Simba fainali za washindi CAF.Kumbukeni pia kocha marehemu Sianga aliifikisha Simba kwenye makundi klabu bingwa ya Africa.Pia marehemu kocha Paul West Gwivaha aliifikisha Simba robo fainali klabu bingwa Africa 1974 ilipotolewa Mehalla ya Misri.
    Sikatai Klabu kuwa na makocha wa kigeni lkn ni muhimu sana kuangalia historia ya makocha waliofundisha Kwa mafanikio na kuwa na uzoefu wa soka la Africa.Binafsi naona Yanga wamefanya uamuzi nzuri Kwa kumuajiri kocha Cedric Kaze na ninaamini atawapa mafanikio.Kocha Sven ni kama anajifunza kufundisha soka ndani ya Africa.
    Simba ingeangalia makocha wenye uzoefu wa kufundisha soka Africa kama kina Cirkovic, Kupunorvic( all ex-coaches Simba),Hans Plujim ( ex Yanga coach),Hubert Vervud( ex TP Mazembe coach),Micho n.k.
    Tuangalie mfano mwingine na tujiulize Kwa nini Al Ahlyi ya Misri imeamua kumchukua kocha Motsime ( ex Mamelod Sundown coach)?

    ReplyDelete
  2. Makocha wetu wazawa wana wakamia makocha wa kigeni wanazozifundisha simba yanga na Azam basi wakitoka hapo wanakwenda kufungwa na ihefu.Lakini mbaya zaidi kwenye mechi za kimataifa ndio maafa zaidi. Hizi simba na Yanga sio kama hazija wahi kuwatumia makocha wazawa.walishawatumia mara kadhaa ila wanafeli.Mfano Yanga imekosa kushiriki kimataifa mwaka huu na mkwasa alikuwepo pale yanga kama ana uwezo huo angethibitisha ubora wake kwenye hii Azam cup baada ya Yanga kukosa ubingwa wa ligi kuu.Kocha bingwa anashnda kunako mechi za kibingwa.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Labda ungeweka kumbukumbu zako vizuri kukosa kwa Yanga Ubingwa mwaka huu Mkwasa alikuwa Kocha msaidizi na walianza kupoteza mwelekeo baada ya kuletwa Mzungu na yeye kufanywa msaidizi

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic