October 5, 2020


 IKIWA kwa sasa Yanga ipo kwenye mchakato wa kumtafuta Kocha Mkuu atakayebeba mikoba ya Zlatko Krmpotic ambaye walifikia naye makubaliano ya kuachana naye Oktoba 3 kutokana na kile kilichoelezwa kuwa ni kutoridhishwa na mwendo wake tayari majina yapo mezani mwa Yanga.


Habari zinaeleza kuwa kwa sasa ndani ya Yanga kuna majina mengi ambayo yanafanyiwa uchunguzi wa sifa za makocha hao huku ikiwa ni pamoja na orodha iliyopita kabla ya kumtangaza kocha huyo.

Miongoni mwa wanaotajwa kuwa kwenye hesabu za Yanga ni pamoja na George Lwandamina raia wa Zambia ambaye aliwahi kuifundisha Yanga na kuipa taji la Ligi Kuu Bara msimu wa 2016/17.

 Kaze Cedric raia wa Burundi huyu anapewa nafasi kubwa ya kuibukia ndani ya Yanga kwa kuwa mchakato wake ulisitishwa mwishoni kabla ya ligi kuanza kwa kueleza kuwa alikuwa na matatizo ya kifamilia na Ernst Middendorp raia wa Ujerumani.

Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela amesema kuwa mchakato kwa sasa wa kutafuta kocha mpya unaendelea.

7 COMMENTS:

  1. BIG BROTHER AFRICA

    ReplyDelete
  2. Tuleteeni chiken man lwandamina jembe la kazi tuweze kufkia our goals

    ReplyDelete
    Replies
    1. Aliondoka anawadai unafikiri anaweza kurudi tena kwenye njaa

      Delete
    2. Hahahahahahahahahahaha!!!!!! Halafu kila kocha anayetimuliwaa huwa halipwi stahili zake,kuna mwaka hii hali itakuja kutuweka mahali pabaya

      Delete
  3. Mlimtimulia nini na sasa mnamtakia nini. Timuwa leo rejesha kesho

    ReplyDelete
  4. Big brother Jangwani. Sijui nani ataondolewa Jangwani sasa?

    ReplyDelete
  5. Viongozi wanajua kwann umemuondoa kocha kwani Siri ya ya mtungi aujuae kata

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic