FRANK Lukwaro, Ofisa Habari wa Klabu ya Polisi Tanzania amesema kuwa kikosi chao kipo tayari kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Bara leo utakaopigwa majira ya saa 10:00 jioni Uwanja wa Uhuru.
Akizungumza na Saleh Jembe, Lukwaro amesema kuwa wanaamini kwamba ushindi walioupata mbele ya Dodoma Jiji utawapa hali ya kujiamini na wachezaji wataingia uwanjani kwa nidhamu.
Lukwaro amesema:"Tunatambua kwamba ushindani ni mkubwa na kila timu inahitaji pointi tatu hivyo hata sisi pia tunahitaji kushinda kikubwa ni sapoti ya mashabiki.
"Wengi wanajua kwamba msimu huu ligi ni ngumu hilo lipo wazi ila mwisho wa siku nasi pia tunahitaji kuendelea kuyakimbiza malengo yetu ikiwa ni pamoja na kumaliza ligi tukiwa ndani ya tano bora."
Kinara wao wa kutupia ndani ya Polisi Tanzania ni Marcel Kaheza mwenye mabao mawili na fundi wa kutengeneza mipira ya mwisho ni Tariq Seif mwenye bao moja na pasi mbili za mabao.
Anakutana na Hassan Kabunda wa KMC mwenye pasi moja ya bao na ametupia mabao mawili ndani ya ligi.
0 COMMENTS:
Post a Comment