TIMU ya Mbeya City leo Oktoba 24 imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Klabu ya Kagera Sugar kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Kaitaba.
Huu ni mchezo wa kwanza kwa Mbeya City kusepa na pointi tatu kwa msimu wa 2020/21 ikiwa ugenini kwani hata ilipokuwa Uwanja wao wa nyumbani Sokoine mambo yalikwenda mrama.
Mabao ya Mbeya City yalifungwa na Abdurazack Mohamed kwa mkwaju wa penalti dakika ya pili na lile la pili lilifungwa lilifungwa na Siraj Juma dakika ya 24.
Kagera Sugar ilipata bao kupitia kwa Erick Kyaruzi dakika ya 46.
Mbeya City ilimfuta kazi Kocha Mkuu Amri Said Oktoba 20 kutokana na mwendo mbaya wa timu hiyo kwa msimu wa 2020/21.
Kwa sasa ipo chini ya Mathias Wandiba ambaye ni kocha msaidizi wa timu hiyo akiwa ni kaimu kocha mkuu.
Matokeo hayo yanaifanya Mbeya City kutoka nafasi ya 18 iliyokuwa kwa muda wa raundi saba na sasa ipo nafasi ya 16 ikiwa na pointi tano baada ya kucheza mechi nane ndani ya ligi.
Kagera Sugar ipo nafasi ya 15 ikiwa imecheza mechi nane kibindoni ina pointi zake tano pia tofauti ya mabao ya kufungwa na kufungana.
Ihefu imeshuka mpaka nafasi ya 18 kwa sasa ikiwa na pointi nne baada ya kucheza mechi nane mchezo wake wa leo imetoshana nguvu ya bila kufungana na Namungo FC kwa kushindwa kufungana.
0 COMMENTS:
Post a Comment