October 24, 2020

 


AZAM FC imetamba kuendeleza dozi kwa timu kongwe za Simba na Yanga kwa kusema kila mechi wanayocheza kwao ni fainali na kudai kuwa siri ya mafanikio ya timu yao ni kutokana na mabadiliko waliyoyafanya msimu huu kuanzia mazoezi hadi usajili.

 

Azam FC inaongoza msimamo wa ligi hadi sasa kwa kushinda michezo saba iliyocheza hivyo kufikisha pointi 21 huku ikizipiku timu kongwe za Yanga ambayo ina pointi 16 na Simba yenye 13.


Ofisa Habari wa Azam FC, Thabiti Zakaria ‘Zaka Zakazi’ aliliambia Championi Jumamosi kuwa: “Kila mechi tunayocheza kwetu ni fainali ikiwemo ya Simba na Yanga, kuna baadhi ya mambo hayakuwa sawa msimu uliopita hivyo tumeyafanyia kazi na ndio maana matokeo yamekuwa hivi.

 

“Lipo suala la wachezaji kujitoa katika kila mechi na si kudharau mchezo wowote baada ya kuona wamepata ushindi katika mechi yoyote.


"Kila mechi kwetu tunaichukulia kama fainali, hivyo tunasahau matokeo ya mechi zetu saba tulizoshinda.


“Sasa tunaangalia mchezo unaofuata dhidi ya Mtibwa Sugar ambao kwetu tunauchukulia kama ni mchezo wa kwanza kabisa, tunahitaji ushindi, lengo letu ni kuweza kutwaa ubingwa msimu huu.

 

“Kuna vitu ambavyo tumevifanyia kazi likiwemo suala la kujituma, matumizi ya viwanja yamekuwa ni sahihi kwa wachezaji kufanya mazoezi sehemu mbili katika kiwanja cha nyasi bandia na uwanja wa kawaida.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic