October 4, 2020


 KUNA kauli kadhaa zimekuwa zikitolewa na watu mbalimbali hasa makocha wa kigeni waliobahatika kufundisha soka hapa nchini wakisema kwamba, Watanzania wengi wanajifanya makocha na kukusoa hata pasipohitaji kukosolewa.

 

Kauli hiyo unaweza kusema ni kama ya utani, lakini ina ukweli ndani yake kwa sababu makocha wengi wanapata shida, si wazawa wala wa kigeni.

 

Kufundisha soka ni kazi kubwa sana, makocha wengi wanapitia wakati mgumu hasa wanapopanga kikosi kwa ajili ya mechi, wakati mwingine hata kwenye kufanya usajili.

 

Ukiangalia usajili uliofanywa na timu kadhaa za hapa nyumbani kabla ya kuanza kwa msimu huu, wapo ambao walikosoa, pia walipongeza kwa baadhi ya sajili. Lakini kubwa zaidi ni kwenye kukosoa.

 

Kukosoa huko kumekuwa kukiendelea kila kukicha. Hata viongozi wa klabu nao wanakumbana na changamoto hiyo hasa pale wanapomleta kocha ambaye kwa muda mfupi anaonekana hafai mbele za macho ya watu.

 

Kulikuwa na kelele za chini kwa chini juu ya aliyekuwa  Kocha Mkuu wa Yanga, Zlatko Krmpotic kwamba hafai kutokana na aina ya ufundishaji wake ndani ya timu.

Hapo ndipo ambapo unaweza kuangalia ni wapi ambapo kulikuwa kunapitisha hizo kelele za chinichini, mfereji wa makosa ya kujirudia na kuanza kuvurugana unaaswa uzibwe ili kuleta maendeleo ndani ya soka la Bongo.


Mvurugano unapoanza mapema mwisho huwa hauwi mzuri kwa sababu kila mmoja atakuja na mbinu zake ambazo zinaweza kuchukua muda mrefu kuzoeleka.


Kocha Msaidizi wa Yanga, Juma Mwambusi kwenye mahojiano yake alikuwa anasema kwamba kupata matokeo ya mabao finyu sababu ilitokana na maandalizi ya muda mfupi.


Hivyo hapo ndipo pa kupatazama vizuri hata kwa yule ajaye pia isije kuwa mwendo ni uleule wa zile kelele.

Licha ya kwamba timu ilikuwa inashinda, lakini haichezi soka la kuvutia. Hapa mashabiki wanataka kuona soka la kuvutia, hawajali sana matokeo. Hii inashangaza kweli.

 Na tayari ameshafungashiwa virago huku sababu ikiwa haijawekwa wazi. Ni maisha ya soka namna yalivyo na hamna namna lazima maisha yaendelee kwa kuwa wamekubaliana wenyewe.

Kuna wakati unaweza kukuta timu inacheza vizuri, lakini suala la matokeo linakuwa mtihani kwao. Nawakumbusha kidogo ilivyokuwa kwa Arsenal chini ya Kocha Arsene Wenger. Kuna kipindi ilikuwa inacheza soka la kuvutia, lakini haina mafanikio.

 

Kikubwa hadi sasa mashabiki wengi huwezi kufahamu wanataka nini hasa. Unaweza kuifanya timu icheze vizuri, wakakupigia kelele wanataka ushindi.

 

Ukianza kucheza soka la kusaka ushindi, utaambiwa tunataka na burudani. Ukiviweka vyote kwa pamoja, watakuja na sera kwamba tunataka mchezaji acheze. Ilimradi wakutikise tu.

 

Nimeanzia mbali lakini pointi yangu kubwa ni kwamba, kikosi cha Taifa Stars kimetangazwa, wapo ambao wameanza kuwanyooshea vidole wachezaji waliochaguliwa na Kocha Mkuu, Ettiene Ndayiragije.

 

Tunatakiwa tufahamu kwamba Taifa Stars ni timu ya Watanzania wote, walioitwa tunatakiwa kuwapa sapoti inayotakiwa ili tu kuipa mafanikio timu.

 

Tukianza kuwabagua kwa kuwapa sapoti baadhi na wengine kuwatenga, hatutakuwa na timu bora kwa sababu wachache wataingia unyonge na kushindwa kupambana.

 

Taifa Stars inapokwenda kucheza mechi ya kirafiki, ndiyo muda sahihi wa kuwatazama wachezaji wetu wote kabla ya kufika mechi za kimashindano.

 

Mechi hizi za kirafiki huwekwa kwa lengo la kuviweka sawa vikosi vyetu. Linapokuja suala la mashindano, huo ni wakati wa kushindana na si kujaribu wachezaji.

 

Tumuachie kocha afanye kazi yake ipasavyo, tusijifanye makocha wakati hatuna taaluma hiyo na hata kama unayo, mwachie aliyepewa dhamana ya kuiongoza timu husika.

 

Ni wazi binadamu kila mmoja ana mawazo na maono yake, ukiangalia Tanzania ina wachezaji wengi tena wa viwango vya juu, tunatakiwa kumuachia kocha anapowachagua wachache, tuwaunge mkono.

 

Kila la heri Taifa Stars katika maandalizi yenu kuelekea mechi hiyo ya kirafiki, kufanya kwenu vizuri ndiyo maandalizi bora kuelekea michezo ya kufuzu Afcon na Kombe la Dunia kwa wakati mwingine. 

9 COMMENTS:

  1. Saleh, mbona timu ya Taifa inakutana siku nne tu na inacheza kwa maelewano? Yule sio kocha. Yanga hii inahitaji Kocha kijana mwenye falsafa za kisasa za soka. Hao wazee wamesoma ukocha miaka ya sabini na themanini hawawezi kuendana na soka la kisasa. Hata Mwambusi hafai pale yanga. Kocha msaidizi angekuwa Said Maulid.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Duh kazi ipo.Ni bora Yanga wakamrejesha babu Hans Plujm ambaye anafahamu soka letu la bongo na bahati baadhi ya wachezaji na kocha Mwambusi alio kuwa nao bado wapo Yanga lkn bado ni kucheza kamari.Rejea pale Simba ilipocheza kamari ya kumrudisha kocha Patrick Phiri na yaliyotokea hakuna aliyeamini na hadi kumpoteza Hamis Tambwe.Kizingiti cha babu Plujim naye haendeshwi kwa remote control.Tumeshaona makocha wengi wa kigeni hawapendi kufundisha timu kwa mihemko ya mashabiki wanavyotaka.Lakini mashabiki tunashindwa kuelewa ktk soka, kocha anahitaji kwanza ushindi na biashara ya burudani baadaye hivyo sioni tatizo la kocha Zlatko ambaye amekuwa na timu kwa takribani mwezi mmoja.Viongozi wanapaswa kumpa ushirikiano kocha kuliko kusikiliza miluzi mingi ya mashabiki isiyoleta tija.Vinginevyo mtabadili makocha atakeyekuja na falasafa yake na usishangae anakueleza Kisinda, Carlihons n.k. hawawezi mifumo yake hivyo dirisha dogo anahitaji wachezaji wengine...sasa hapo itakuwa faida au hasara kwa timu kusajili lundo la wachezaji kama ilivyotokea kina Balinya kusepa zao.

      Delete
  2. Ha!ha!haaa! Kijana anataka pesa mnazo? Vibabu ndo saizi yenu

    ReplyDelete
  3. Wabongo wanaongozwa wanaojiita wawakilishi/kioo cha jamii wanaandika habari kwa ajili ya kuuza tuu bila kujali matokeo ya habari hiyo inaathiri jamaa kiasi gani. Kuna wakati habari inataja mtu wakati ni uongo mtupu lkn wahusika wanakaa kimyaaa. .... kila kukicha kukosoa klabu na mienendo yake.

    ReplyDelete
  4. Hapa huyo Hersi na wenzake wajuwe hata Yanga I cheze vipi hatakuja kufurahisha Media cse 80 to 90 percent Ni wa upande wa pili .Yanga inatumika tu kwa biashara tu,bt majority Waandishi/Watangazaji nk ni wale wale na kwa mbia Kama hakujua hata Mwamnyeto kuja Yanga haikufurahisha media.Shida msiojua kufahamu makala na content zake wengi ni Yanga mna bore.Timu inaanza kuonekana mnafukuza Kocha kwa lipi mnalotegemea ku achieve kwa haraka.INASIKITISHA.LEO MWISHOOO wangu kushabikia huu upuuzi na namuomba Mungu anitoe nyongo ya kupenda Mpira wa Tanzania mnafanya the same mistake kwa pressure ya Nani au mna deal kwenye KU recruit new Coaches?Aminaaaa

    ReplyDelete
  5. Sasa nimeanza kuona kipaji Cha Senzo Masingiza

    ReplyDelete
  6. SENZO namuelewa sana, hapa usishangae analetwa GAUDIOLA u ZIDANE

    ReplyDelete
  7. Utopolo senzo anawatafutia kocha mkaliii, vumilieni tu msijihudhuru kuishabikia team yenu mmeipenda na mmeitaka wenyewe acheni iwatese tu.

    ReplyDelete
  8. bongo kila mtu kocha kila mtu mchambuzi hahahhaha

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic