October 11, 2020

 


KOCHA Mkuu wa Yanga, Cedric Kaze ambaye anapenda soka la pasi za chini anatarajiwa kuwasili nchini Tanzania Oktoba 15 kuanza kazi rasmi ndani ya kikosi hicho.

 Kaze ambaye habari zinaeleza kuwa anakuja kubeba mikoba ya Mserbia, Zlatko Krmpotic aliyesitishiwa kibarua chake Oktoba 3 muda mfupi baada ya kumaliza mchezo wake wa ligi dhidi ya Coastal Union kwa sasa yupo Canada.


Kwenye mchezo huo, Zlatko alishinda mabao 3-0 na kufanya uwe mchezo wa kwanza kwa Yanga kushinda mabao mengi ndani ya Ligi Kuu Bara kwa kuwa mechi zake nne alizokaa benchi alifunga bao mojamoja.


Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Kampuni ya GSM ambao ni wadhamini ndani ya Klabu ya Yanga, Injinia Hersi Said amesema kuwa kila kitu kinakwenda sawa na kocha anaweza kuwasili Bongo Oktoba 15.


"Bado mchakato wa kumleta kocha mpya unaendelea na kwasasa tupo kwenye hatua nzuri ambapo kuanzia wiki hii ya kesho atakuwa ameshawasili nchini.


"Ninadhani Oktoba 15 ambayo ni Alhamis anaweza kuwasili Tanzania rasmi kwa ajili ya kuendelea kukinoa kikosi ambacho kipo kambini kwa sasa," amesema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic