KIKOSI cha timu ya Azam Media jana Oktoba 10 kilifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 4-1 kwenye mchezo wa kirafiki uliochezwa Uwanja wa Karume, Ilala, Dar.
Mchezo huo
ambao ulikuwa maalumu kwa ajili ya kuwahamasisha mashabik kujitokeza kwa wingi leo
Oktoba 11, Uwanja wa Mkapa ulihudhuriwa na mashabiki wengi waliojitokeza kuona
burudani ndani ya uwanja.
Kipindi cha
kwanza timu zote mbili zilikwenda mapumziko huku Azam Media ikiwa mbele kwa
mabao 2-1 jambo lililowavuruga wachezaji wa Global FC waliokuwa wamejipanga
kupata matokeo chanya
Kipindi cha
pili kilikuwa na ushindani mkubwa na Azam Media iliweza kufunga mabao mawili
mengine na kuwafanya wawe mbele kwa
mabao manne.
Mpaka dakika
90 zinakamilika Uwanja wa Karume, Azam Media ilikuwa inaongoza kwa mabao 4-1
huku Global FC ikiwa na bao moja pekee ambalo lilikuwa la kufutia machozi.
Ushindi huo
unawafanya Global FC kurejea chimbo upya kuanza kujiandaa kwa mchezo wa marudio
dhidi ya timu ya Azam Media ambao unatarajiwa kuchezwa hivi karibuni.
0 COMMENTS:
Post a Comment