UONGOZI wa Mtibwa Sugar umesema kuwa utatibua rekodi ya Azam FC ya kucheza mechi saba bila kufungwa kwa kuwa wamejipanga kupata ushindi kwenye mchezo wao wa ligi utakaochewa Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.
Kwa sasa Azam FC ni vinara wa ligi wakiwa na pointi 21 baada ya kucheza mechi saba msimu wa 2020/21 na kimefunga jumla ya mabao 14.
Kinara wa mabao kwa msimu huu ni Prince Dube wa Azam FC ambaye amefunga mabao sita na ana pasi nne za mabao.
Thobias Kifaru, Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar amesema kuwa kwa sasa kikosi kimejipanga kufanya vizuri na wana imani watapata ushindi mbele ya Azam FC inayonolewa na Aristica Cioaba.
"Kila kitu kinakwenda sawa nina amini kwamba uwezo upo na tunahitaji pointi tatu kwenye mechi zetu ambazo zinatukabili ikiwa ni pamoja na ile dhidi ya Azam FC.
"Tunajua kwamba haijapoteza mpaka sasa lakini sisi tutashinda na kuvunja mwiko ambao umewekwa na wapinzani wetu hasa ukizingatia kwamba tutakuwa nyumbani, mashabiki wajitokeze kwa wingi," amesema.
Mtibwa Sugar ikiwa chini ya Vincent Barnaba mchezo wake wa mwisho ilishinda bao 1-0 dhidi ya Namungo na inakutana na Azam FC ambayo imetoka kushinda mabao 2-0 dhidi ya Ihefu FC.
Sawa MCHEZO utakaochezwa uwanja wa JAMHURI kwa siku gani sasa, mbona habari yako haijakamilika
ReplyDeleteMara nyingi hii kitu waandishi huwa hawaandiki sijui wanafeli wap
DeleteTatizo wanaandika kwa kufikiria kila mtu anajua mchezo unachezwa linit
Delete