October 9, 2020

 


LAMINE Moro, nyota wa Yanga, raia wa Ghana leo Oktoba 9 atakuwa na kazi ya kwanza kukiongoza kikosi chake kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Mwadui FC, akiwa ni nahodha kamili.


Kitambaa hich alipewa rasmi jana, Oktoba 8 ambapo awali kilikuwa kinavaliwa na mzawa Deus Kaseke, Haruna Niyonzima na Moro mwenyewe.

Tshishimbi alikuwa nahodha mkuu wa mwisho katika kikosi hicho mpaka msimu uliopita unamalizika lakini baadaye aliachana na klabu hiyo baada ya kushindwa kukubaliana na viongozi wa klabu hiyo katika kuongeza mkataba mpya.

Moro ambaye tayari ana uhakika wa kuendelea kukipiga ndani ya Yanga baada ya hivi karibuni kuongeza mkataba wa kuendelea kusalia katika klabu hiyo kuwa nahodha wao mpya akiwa ameanza vyema msimu huu.

 

Mbali na Moro pia beki mwenzake pacha Bakari Mwamnyeto naye amepewa unahodha msaidizi katika majukumu hayo.


Mabeki hao ndio wanaongoza safu ya ulinzi ya Yanga ambayo mpaka sasa katika mechi tano ndio ukuta pekee umeruhusu bao moja pekee huku pia Moro akifunga mara mbili katika mechi mbili tofauti.


Pia taarifa hiyo imemtaja kiungo Mukoko Tonombe kuwa nahodha wa tatu akimsadia Moro ambapo mkongomani huyo akiwa ameanza vyema msimu huu wake wa kwanza ndani ya Yanga akiwa na bao moja huku pia akitoa pasi moja ya bao.

 

Hatua hiyo ya Yanga ni kama inawaongezea morali zaidi wachezaji hao watatu wanaocheza eneo la ulinzi katika kuiongoza timu hiyo kuwa bora zaidi katika ukuta wao msimu huu ambao hawajapoteza mechi yoyote zaidi ya kutoa sare moja na kushinda mechi nne.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic