October 28, 2020


 KATIKA hali ya kushangaza mshambuliaji wa Simba, John Bocco, juzi alinusurika kupigwa na mawe na mashabiki wa timu hiyo kufuatia kitendo cha kukosa penalti katika mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Ruvu Shooting ambao walichapwa bao 1-0.

 

Bocco alikosa penalti dakika ya 78 kwa shuti lake kugonga mwamba hali ambayo iliwakasirisha mashabiki kwa kuwa mchezo uliopita walifungwa bao 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons.


Championi ambalo lilikuwepo uwanjani liliwashuhudia mashabiki wakiwa wamejazana upande wa kutokea uwanjani huku wakidai wanamtaka Bocco na wengine wakiwa wameshika mawe mkononi.

 

Kitendo cha mashabiki hao kilipelekea Polisi kulazimisha basi la timu hiyo kuingia ndani ya uwanja kwa lengo la kuwatoa wachezaji huku ulinzi ukiwa umeimarishwa lakini haikuweza kuwafanya mashabiki hao kutoka katika eneo.


Hata hivyo basi la timu hiyo liliwachenga na kupitia kwenye geti lingine linalotazama na Uwanja wa Mkapa na kuondoka uwanjani hapo.

8 COMMENTS:

  1. Ndio tabu ya sisi mashabiki hawaelewi, kuwa "kupata penalty ni jambo moja, na kufunga jambo lingine " pole bocco wavumilie watasahau tu

    ReplyDelete
  2. Ndio tabu ya sisi mashabiki hawaelewi, kuwa "kupata penalty ni jambo moja, na kufunga jambo lingine " pole bocco wavumilie watasahau tu

    ReplyDelete
  3. Uongo mtupu,hakukuwepo na tukio la namna hiyo,hawa vilaza wanaandika habari za kufikirika ili kujaza kurasa na kufurahisha nafsi zao

    ReplyDelete
  4. Mtapigana sana tu mwaka huu nyie manyumbu fc

    ReplyDelete
    Replies
    1. Churaaaa fc furaha yako ni kama umeme wa lUKU hatuna haja ya kubishana na wewe

      Delete
  5. habari za hawa jamaa hua za kuunga unga sana

    ReplyDelete
  6. Naona Simba wanaielewa rangi adimu ya Yanga@njano

    ReplyDelete
  7. Duh!kupoteza mechi mbili tu kizaazaa kimeanza

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic