October 5, 2020

 


PIUS Buswita, kiungo mshambuliaji wa Klabu ya Polisi Tanzania ambaye leo ameibuka shujaa kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Uhuru wakati wakishinda bao 1-0 dhidi ya KMC amesema kuwa ushindi huo unatokana na maelekezo kutoka kwa mwalimu.

Bao pekee la ushindi lilipatikana dakika ya 88 baada ya dakika 45 za mwanzo kukamilika bila kufungana na kipindi cha pili mambo yalikuwa maguku kwa timu zote mbili na mwisho wa siku Buswita aliibuka shujaa.


Akizungumza na Saleh Jembe Buswita amesema kuwa ulikuwa ni mchezo mgumu na wenye ushindani kwa pande zote mbili kabla ya kusepa na pointi tatu.


"Ulikuwa ni mchezo wenye ushindani na kila timu ilikuwa inahitaji ushindi ila mwisho wa siku tumeweza kupata matokeo na ni furaha kwetu.


"Ni zawadi yangu kwangu na timu ukizingatia leo ni siku yangu ya kuzaliwa najua wachezaji wenzangu wamefurahi hata mimi nimefurahi pia," amesema.


Ushindi huo ni wa pili mfululizo kwa Polisi Tanzania baada ya kutoka kushinda kwa mabao 3-0 mbele ya Dodoma Jiji huku KMC ikipotza mchezo wake wa pili baada ya kutoka kufungwa bao 1-0 mbele ya Kagera Sugar. 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic