MASHABIKI wamelinganisha kasi aliyoanza nayo mfungaji bora wa Ligi Kuu Bara msimu uliopita, Meddie Kagere na hii aliyoanza nayo straika mpya wa Azam, Prince Dube msimu huu, na hapo ndipo Championi Ijumaa lilipoamua kuingia mzigoni kujua nani alianza kwa kasi zaidi.
Katika mechi saba za kwanza msimu uliopita, Kagere, raia wa Rwanda, alihusika kwenye mabao tisa kati ya 12 ambayo Simba ilifunga kwenye mechi hizo, akifunga mabao saba na kutoa asisti mbili.
Dube ambaye huu ni msimu wake wa kwanza ndani ya Ligi Kuu Bara, tayari ameivunja rekodi hiyo ya Kagere akihusika kwenye jumla ya mabao 11 kati ya 14 yaliyofungwa na timu hiyo katika mechi saba za kwanza hadi sasa.
Hii inamaanisha kuwa Kagere atakuwa na kazi kubwa ya kutetea kiatu chake kama Dube ataendeleza kasi yake hiyo hadi mwisho wa msimu.
Dube msimu huu amefunga mabao sita na kutoa asisti tano.Dube mechi alizofunga ni dhidi ya Coastal Union mabao mawili, Prisons (1), Kagera (2) na Mwadui (1).Akatoa asisti moja dhidi ya Polisi Tanzania, Ihefu (2), Mwadui (1) na Kagera (1).
Kwa upande wa Kagere, alizifunga JKT Tanzania mabao mawili, Mtibwa Sugar (1), Kagera Sugar (2), Biashara United (1) na Azam (1), huku akitoa asisti hizo mbili dhidi ya Biashara na Kagera Suga
Habari ya mujini Ni Prince Dube
ReplyDelete