BAADA ya mchezo wa jana Oktoba 22 kwa kufungwa bao 1-0 kikosi cha Simba kimeanza safari leo kurejea Dar kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Ruvu Shooting.
Simba ilifungwa bao hilo kwa kichwa na Samson Mangula dakika ya 49 na kuwafanya mabingwa hao watetezi kuziacha pointi tatu Uwanja wa Nelson Mandela.
Mchezo wao dhidi ya Ruvu Shooting utachezwa Uwanja wa Uhuru, Oktoba 26 saa 10:00 Uwanja wa Uhuru.
Kocha Mkuu wa Simba Sven Vandenbroeck, amesema kuwa kilichotokea ni sehemu ya mchezo hivyo watatumia makosa waliyoyafanya kufanya vizuri mchezo ujao.
"Kilichotokea mbele ya Prisons ni sehemu ya mchezo, kwa sasa tunaelekeza nguvu zetu kwenye mchezo wetu ujao dhidi ya Ruvu Shooting," amesema.
Simba ipo nafasi ya tatu ikiwa na pointi 13 baada ya kucheza mechi sita ndani ya ligi, kinara ni Azam FC mwenye pointi 21 baada ya kucheza mechi saba na watani zao wa jadi Yanga wapo nafasi ya pili wakiwa na pointi 16.
Ujinga mtupu kwa staili hii ubingwa tusahau labda nafasi ya 3 tena labda kila kitu wanapewa wasafiri kwa ndege wanalipwa vizuri ujinga mtupu
ReplyDeleteLigi bado hata haijafikia robo ya mechi zote. Msimu uliopita kwani Simba hawakufungwa? Walifugw ana ubingwa wakauchukua
DeleteUsihofu sana Simba ina kikosi kipana, ni ya level nyingine. Ina wachezaji kama akina Bernard Morrison wanaoweza kukupa matokeo wakati wowote!
DeleteWw hujui mpira unafikiri kila siku J2, mpira Ni ushindani ukiingia ovyo unapigwa ujipange upige hatua maana hakuna atajayeshindwa mechi zote Leo Simba kesho mwingine ndo mpira huo
DeleteHivi kilicho sababisha Mugalu asicheze jana ni kitu gani jamani; maana hao akina Chama tunajua walikua na sababu za kutokuwepo
ReplyDeleteAlitonesha jeraha kwenye mazoezi kabla ya mechi. Jeraha alilipata kwenye mechi ya kirafiki na Mlandege
DeleteMugalu aliumia kwenye mazoezi ya mwisho lakini Simba hawakutaka kutoa taarifa kuhofia pressure kwa mashabiki
ReplyDeleteHivi ni nani aliyewaambia Simba na Yanga hazistahili kufungwa?
ReplyDeleteKocha huyo alisema akifikisha mechi Hadi 7, Simba watakuwa wanaongoza ligi, imebaki mechi moja, naona hyo Simba akimshinda atapewa point 6 ili aongoze ligi
ReplyDeleteHapa wapendwa ndiyo tunaona utamu wa Ligi na kufungwa Simba siyo shida mbona Liver alichezea kwa Aston Villa Tena kichapo Cha kukera
ReplyDeleteTahadhari hapa ni baadhi ya Timu na Viongozi wenye tabia za kutumia njia za Panya kulazimisha ushindi hasa pale matokeo yanapowapiga vibaya.Kufungwa ni kitu Cha kawaida hapa Ni kujipanga kwa Mechi hijayo siyo kuanzisha Kamati za Fitna(football) tutulie tusiharibu ligi.
OVYOOO :Wamekalili mech za 'away" ni kufungwa tu hii simba au utopolo ??
ReplyDeleteKikosi cha mabilion kufungwa na askari magereza wanaolipwa posho
Wanashndwa mpira wananenepa makalio tu
Utopolo ni yanga usibadilishe jina
DeleteUtopolo Ni yeboyebo na jina mlijipa wenyewe nanikweli ninyi Ni utopolo.
ReplyDeleteSimba ni 'mikia','mtepeto, mikia kupinda'
DeleteUnajua maana ya mkia ww kiazi, Nani bingwa wa nchi mpaka hivi sasa. Hujui tafsiri ingia darasani kwenye jamii acha kukaa nyara
DeleteMbona simba mmejaa mihasira ovyo mkubali mlikula kichapo na kupigishwa gwaride na wanao jua kucheza mpira wa uwanjani sio wa mdomoni aaahahahaaaa haooo bichwa limeachama wamemeza inzi wa chooni
ReplyDelete😄😄😄 Simba anahasira na makombe, tutayakusanya mengi tu.
Delete