KUUMIA kwa beki wa kulia wa Simba, Shomari Kapombe jana Oktoba 22 kunafanya jumla ya wachezaji watano wa Simba kuwa majeruhi.
Nyota mwingine ambaye ni majeruhi ni Chris Mugalu, raia wa Congo ambaye alipata maumivu ya nyonga muda mfupi kabla ya timu hiyo kuvaana na Tanzania Prisons.
Wengine ambao ni majeruhi ni pamoja na Meddie Kagere na John Bocco ambao wote ni washambuliaji.
Pia Gerson Fraga, kiungo wa Simba pia naye ni majeruhi ambapo aliumia wakati timu ilipokuwa ikipambana na Biashara United.
Simba ilipoteza mchezo wake wa kwanza wa ligi kwa kuchezewa gwaride na Tanzania Prisons ambao walisepa na pointi tatu jumlajumla Uwanja wa Nelson Mandela.
Daktari wa Simba, Yassin Gembe amesema kuwa kwa sasa ni ngumu kuzunguzia hali za wachezaji hao wakikamilisha utaratibu watatoa taarifa kupitia vyombo vyao vya habari.
Pole yao wagonjwa tunawaombea kupona haraka. Lakini pia hii inaonesha Simba hawana kikosi kipana kama tunavyoaminishwa na msemaji maarufu hapa nchini. Ni vema akatengua hiyo kauli ya "simba inaweza kuchezesha timu mbili tofauti na zote zikashinda!!!" Kwa matokeo ya wajelajela na ya wanasukari nadhani bado kabisa Simba hawajajipanga kimataifa na wasipofuata ushauri wa Zahera kuna aibu huko mbele inakuja ya khamsa khamsa.
ReplyDeleteKwani umeambiwa ukiwa na kikosi kipana ndo hufungwi, acha ushamba wewe..... Huko kimataifa Utopolo mtasubir Sana maana hata huyo kaze naona mpira ni ule ule tu wa kocha aliyepita anachojitahidi ni kuwajaza maneno tu Ila hamna kitu.
ReplyDeleteMisukule mbona hamtaki kuambiwa ukweli.....gwaride mmepigiwa afu bado midomo mirefu Kama magali ya mwendokasi......acheni kulalama huyo nguruwe wenu si ndo kashawaaminisha kuwa Simba inaweza kucheza michezo miwili kwa wakati mmoja na mkashinda....shindeni Sasa kwa wajelajela.....afu niwaambie tu.....kuna bomu linakuja Sema ni swala la muda tu
ReplyDeleteHongereni utopolo mshatwaa ubingwa.
ReplyDelete