KIKOSI cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck, leo Oktoba 2 kimeanza safari kwa basi kuelekea Morogoro ambapo kitapeleka taji la Ligi Kuu Bara kwa mashabiki wake wa Moro ambao waliomba wapelekwe.
Taji hilo ambalo ni la tatu kwa Simba ni la kwao jumla kwa mujibu wa kanuni walilitwaa msimu wa 2019/20 hivyo kwa msimu huu wa 2020/21 ni mabingwa watetezi.
Kabla ya kuondoka asubuhi ya leo wachezaji walifanya mazoezi ikiwa ni maandalizi ya kujiweka sawa kuelekea mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya JKT Tanzania unaotarajiwa kuchezwa Oktoba 4, Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.
Leo kikosi kitaweka kambi Morogoro na kesho kitaanza safari kuelekea Dodoma, makao makuu ya nchi kwa ajili ya maandalizi ya mwisho kabla ya kumenyana na JKT Tanzania.
Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa wanawapelekea taji mashabiki wao wa Moro ili kutimiza ombi lao ambalo uongozi unaliheshimu na kulifanyia kazi kwa ukaribu.
0 COMMENTS:
Post a Comment