October 3, 2020

 


UONGOZI wa Simba umesema kuwa uwezo wa kiungo mkabaji Said Ndemla ndani ya Simba kwa msimu wa 2020/21 ni moja ya sababu ya yeye kuitwa kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania,  Taifa Stars.


Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa timu ya Taifa ya Tanzania haitazamani rekodi za miaka nane ama sita ila wanatazama kile ambacho amekifanya kwa muda akiwa ndani ya Uwanja kwa wakati huo.


Ndemla ni miongoni mwa nyota ambao wametajwa kwenye kikosi cha  Stars kitakachoingia kambini Oktoba 5 kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya Burundi unaotarajiwa kupigwa Oktoba 11, Uwanja wa Mkapa. 


Manara amesema:"Kwa namna ambavyo Ndemla anafanya juhudi na uwezo alionao anastahili kuitwa kikosi cha Stras, ni mtu anayepata namba kikosi cha kwanza na anapambana kufanya kazi makini sasa kwa nini asiitwe kwenye kikosi? 


"Kupata namba ndani ya kikosi cha Kwanza Simba sio kitu chepesi kwa kuwa kikosi ni kigumu na kina kila aina ya wachezaji wazuri, Ndemla atafanya makubwa kwa kuwa anapata namba ndani ya Simba," amesema.

8 COMMENTS:

  1. dogo yuko vizuri.. tunajua kuna watu wanakereka.. wamewekeza mabilioni lakini mambo ni yale yale mfano kila mechi kushinda ni shughuli kagoli kamoja kuanzia dakika ya 70 ndiyo linapatikana...ni ile ile kama ya wakati wa kocha zuhura na kocha mbaguzi..pia ni ile ile kwani wakiitwa Stars kikomo ni wanne to..wanakaa kuchunguza mikataba ya timu jirani na ya wachezaji wasio wao..Ushauri wekezeni bilioni 2 hapo mtafanikiwa!

    ReplyDelete
  2. Kwahiyo Simba ndiyo inaytoa maelekezo kwa Kocha wa Taifa kuchagua Wachezaji ? Inapendeza.LKN mimi nashauri na kueleza kama si kuelewa kweli kwa sisi Wakristo ,kwanini Mungu alichagua Wayahudi/Waisrael Kama Taifa au kabila lake.Liverpool bingwa wa Wingereza kwa tofauti ya Pointi 18 . Southgate kachagua Wachezaji 3 tu.

    ReplyDelete
  3. Liverpool
    vs
    utaifa
    Salah
    si
    muingereza
    wala
    Mane

    ReplyDelete
  4. Wewe kwani Hiyo Simba regular players si wanajulikana? Wa ndani always Manula, Kapombe,mmed,Mkude,Bocco Kama Timu ipo sawa.Mzamiru na Dilunga ,Gadiel sub huyo Ndemla always hacheezi .Leo tu Mechi mbili National Timu
    Na Liverpool regular English players Trent,Gomez,Henderson ,sub Ox Chamberlain,Curtis Jones hapa Swali Kama unafunga Gwambina yenye full Local players wewe umejaza foreigners 2/3 if not3/4 na baada ya hapo unasifia Sambusa kwanini ujisidie kufunga Timu ambayo haina Wachezaji wenye hadhi na je Ni kweli hizo Time wachezaji wao siyo Wazuri wakucheza National Team ?Ukizingatia game nyingi Zina maamuzi Tata.Na je kweli Team ya Taifa inajengwa hivyo?

    ReplyDelete
  5. Jaman cc wanayanga tunafunga goli 1 ndio lakin cmba goli 4 kwa gwambina na biashara kwa mtibwa wakafunga 10 ihefu wakafunga 15 lakin wapo na point ngap? Na yanga tunangap? Unapotoa comment angalau ufikie kwanza .mwisho sio kila aitwae kwenye taifa ndo atacheza

    ReplyDelete
  6. Kwani walofunga Magoli mengi KMC wameitwa halafu zaidi wote wazawa na mmoja amentesha kulinda Kiwango alikuwa na goli 13 Mwaka Jana ana mbili mwaka kwa michezo miwili je Bocco ana ngapi na mwaka Jana alifungwa ngapi ?Ok cse Ni friendly na si lazima kila anayeitwa acheze kwanini ung'ang'anie Wachezaji wa Timu moja ,usiwape exposure hata akina Lusajo?Mimi najua haya ni matakwa ya Watu fulani ukweli kwa hii Mechi hata hao akina Samatta hapakuwa na umuhimu wa kuwaita ,kwa staili tutapiga jaramba Sana.Ila argue kwa mapana usilenge Yanga,Kama kweli unajisifia kufunga Goal nyingi against Gwambina& Biashara u mean hizi Team Zina Wachezaji Wazuri , Sasa mbona hawaitwi?jibu kwa hoja usikalili Yanga iwe ndilo jibu lako

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hata ukiangalia bado kuna wachezaji Simba, Yanga, Azam, Kagera etc ni wazuri na wanafaa kuchezea timu ya Taifa lakini hawakuitwa.Mchezaji kuitwa timu ya taifa isiwe kwa majaribio au vinginevyo timu ya taifa itakuwa haipandi chati ya viwango vya FIFA.Kama unadai kina Lusajo waitwe ili wapate exposure basi hakuna haja ya kuitwa kina Samatta,Ulimwengu na wengineo wanaocheza nje ya nchi.Eleweni kuwa hii ni kalenda ya FIFA hivyo ni nafasi ya timu ya taifa halisi ya kuonyesha uwezo wa wachezaji wote ulio nao nje na ndani ya nchi.

      Delete
  7. Magoli ya Simba 7/8 wamefungwa foreigners na 1/8 wazawa na Ni against Ihefu .

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic