October 16, 2020

 


KIUNGO mchezeshaji wa Simba, Mzambia, Clatous Chama, ameweka wazi kwamba licha ya kukosa kucheza na Yanga Oktoba 18, mwaka huu lakini anaamini watazipata pointi zao kutokana na kuongezewa muda zaidi wa kujiandaa.

 

Kiungo huyo ameongeza kwamba walikuwa wameshaanza kuitolea macho mechi hiyo ya dabi lakini kwa sasa wanaangalia mechi zijazo baada ya kupelekwa mbele.


 

Simba walipangiwa kucheza na Yanga kwenye Kariakoo Dabi Oktoba 18 lakini mechi hiyo ya Ligi Kuu Bara imesogezwa mbele hadi Novemba 7.


Kiungo huyo raia wa Zambia amesema kwamba kwa sasa hawana cha kupoteza baada ya kushindwa kucheza na Yanga na wanaangalia mbele katika mechi zao zijazo za ligi.

 

“Simba kila siku iko tayari kwa ajili ya kupambana na timu yoyote ile kwa sababu msimu unaenda mbele.

 

"Mechi na Yanga ni mechi kubwa ambayo tulikuwa tunaiangalia lakini nafikiri sababu za kughairisha mechi zilizotolewa ziko vizuri.

 

“Tuna mechi nyingine hapa kati kama ratiba yetu inavyoonyesha na pale ambapo itakuja tutacheza. Nafikiri imetupa muda zaidi wa kujiandaa, hiyo ni mechi kubwa lakini naamini tutafanya vizuri,” alimaliza Chama.

7 COMMENTS:

  1. Uko usingizini wewe unategemea utaifunga yanga au unawapa moyo

    ReplyDelete
  2. Hivi wewe unayezungumzia kwenye kijiwe cha kahawa na Mwamba wa Lusaka aliyewatungua Yanga na kuwa mchezaji bora wa msimu tumsikilize nani?Wewe unayebisha hata kupiga danadana 3 huwezi. Umekalia kupiga domo.

    ReplyDelete
  3. Kwani hamkufungwa 4 au sio nyinyi? Subiri 5 sasa

    ReplyDelete
  4. Itawakera na bado huyo mlio msainisha mtamuona hafai tena

    ReplyDelete
  5. Nadhani Chama sijui Cuf anaujauzito Mechi Ile mlicheza against 8 players cse Mourrison mlisha mkamata akawa anawasaidia, Tshishimbi na Molinga Hiyo tunasema akhasante mwenye hii blog uli play part ya kuwapumbaza Yanga wawe sehemu ya Mchezo huo ,Kama mlivyojitahidi wakati wa Usajili kuwapigia debe hili waendelee kuwepo mpate upenyo ,huyo Chama zile Mechi tulicheza seroous hakuonekana(za Ligi)hii ya pili(Fa) ilijaa siasa za kuchekesha

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nahisi vyura wa pale matopeni jangwani wameingia kichwani kwako.Unachozungumza ni pumba tupu.Yanga bado wepesi sana labda umuweke kocha Charles Boniface hapo ndio najua kuna kazi ya kumfunga Utopolo alias gongowazi a.k.a.wa matopeni

      Delete
  6. Cse tuliona hata Kamati Tendaji ya Tff na Kamati zake meno yote nje,Sasa hv mkipata hata goli la offside Mimi nakuwa chizi

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic