October 30, 2020


SVEN Vandenbroeck Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa hakuwa na chaguo la kufanya ndani ya uwanja zaidi ya kumtumia Ibrahim Ajibu kuwa mshambuliaji kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Ruvu Shooting wakati wakipoteza kwa kufungwa bao 1-0.


Oktoba 26, Simba ilipokea kichapo cha pili mfululizo ikiwa ni cha pili mfululizo kwa msimu wa 2020/21 baada ya kuanza kufungwa bao 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons.


Kwenye mchezo huo Ajibu alipewa jukumu la kusaka ushindi kwa timu yake akilishwa mipira na Luis Miqussone ambaye ana jumla ya pasi tano na bao moja ndani ya ligi.


Sven amesema:"Sikuwa na jambo la kufanya kwa kuwa washambuliaji wangu wengi walikuwa ni ni majeruhi hivyo sikuwa na chaguo zaidi ya kumtumia Ajibu kwenye mchezo wetu dhidi ya Ruvu Shooting."


Ajibu kwenye mchezo huo alipiga jumla ya mashuti manne ambayo hayakulenga lango.


Simba ambao ni mabingwa watetezi kwa sasa wanajiandaa na mchezo wa ligi dhidi ya Mwadui FC utakaochezwa kesho, Oktoba 31 Uwanja wa Uhuru.

3 COMMENTS:

  1. Mashuti manne ambayo hakuna hata moja lililolenga lango dk 90,halafu asipopangwa mnalalamika wazawa hawa hawajitambui.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ajibu ni Side 10 unapompanga namba 9 ni wa umeuongea na kupunguzanamna ya uchezaji wake...
      Akicheza side 10 yeye anakuwa na nafasi kubwa ya kutengeneza nafasi za kufunga kwa namba 9 wake kwa kupiga pasi za mwisho.....
      Pia akicheaza namba 9 yeye ndiyo anakuwa mtu wa mwisho anaetgemewa kufunga baada ya kupesa pasii..... Swali la kujiuliza uwiano wa wachezaji ulijitosheleza kutengeneza nafasi za magoli

      Delete
  2. Kukosa mshambuliaji siyo ndo umpange ajibu kati, heri ungempanga louis au morrison maana wana kasi ajibu abaki namba 10.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic