USHINDI wa jana Oktoba 4 kwa Azam FC wa mabao 4-2 mbele ya Kagera Sugar uliochezwa Uwanja wa Azam Complex unawafanya Azam FC kuandika rekodi nne matata ndani ya dakika 90.
Rekodi ya kwanza kwao kushinda mabao mengi ambayo ni 4-2 mbele ya Kagera Sugar.
Rekodi ya pili ni kwa David Kisu kutunguliwa mabao mengi ambayo ni mabao mawili kwa kuwa mechi nne alikuwa hajatunguliwa na aliyeanza kumtungua ni David Luhende.
Rekodi ya tatu ni kuwa na kinara wa mabao ambaye ni Prince Dube amefikisha jumla ya mabao 5 na kumshusha Meddie Kagere wa Simba mwenye mabao manne.
Rekodi ya nne kwa msimu wa 2020/21 mechi moja kukusanya mabao mengi ambayo ni sita. Wanarejea kileleni wakiwa na pointi 15
Kwa sasa Azam FC ni vinara wa raundi ya tano kwa mara nyingine tena wakiishusha Simba ambayo ilidumu hapo kwa muda kidogo baada ya kushinda mabao 4-0 mbele ya JKT Tanzania na kufikisha pointi 13.
Kagera ishakuwa jamvi la wageni, Bora ishukd daraja tu
ReplyDeleteUkiona simba anaongoza jua azam hajacheza? Na ukiona kagere anaongoza kwa magoli mengi bc jua dube anagemu mkononi?
ReplyDelete