October 11, 2020

 


MEDDIE Kagere mshambuliaji namba moja ndani ya Simba kwa msimu wa 2020/21 ana kazi ya kufanya kutetea kiatu chake cha ufungaji bora kutokana na ushindani ambao umeanza kuonekana ndani ya Ligi Kuu Bara. 


Mpaka sasa ikiwa ni raundi ya tano Kwenye Ligi Kuu Bara tayari yameshafungwa jumla ya mabao 53 jambo ambalo linamaanisha kwamba msimu huu sio wa mchezo mchezo kwenye vita ya ufungaji.


Katika mabao hayo hakuna hata bao moja la penalti ambalo limefungwa mpaka sasa kwa raundi hizi tano ambazo zimepita na ni moja tu la kujifunga ilikuwa ni Kwenye mchezo kati ya Coastal Union ya Tanga na JKT Tanzania. 


Simba ikiwa imefunga mabao 14, Kagere ambaye ni mfungaji bora wa misimu miwili mfululizo ametupia jumla ya mabao manne kwenye nyavu.


Alitwaa tuzo ya ufungaji bora msimu wa 2018/19 alipofunga mabao 23 na msimu wa 2019/20 alipofunga mabao 22  kazi ya kutetea kiatu hicho imeshaanza.


Mshindani wake mkubwa ni Prince Dube wa Azam FC ambaye Azam FC ikiwa imefunga mabao tisa amehusika kwenye mabao saba ndani ya kikosi hicho.


Amefunga matano akiwa ni kinara wa kutupia na ametoa pasi mbili za mabao kibindoni hivyo kasi ikiwa hivi mpaka mwisho Kagere ana kazi ya kufanya msimu wa 2020/21 kufikia malengo yake ya kutetea kiatu cha ufungaji.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic