BAADA ya kufanikiwa kufunga bao lake la kwanza na kwa mara ya kwanza kwenye Ligi Kuu Bara, beki wa Simba, Pascal Wawa amesema kuwa atafanya kila jitihada ili aendelee kufunga mabao mengine kama ambavyo mabeki wa timu nyingine wanavyofanya.
Wawa alifungua akaunti yake ya mabao kwenye ligi ya Bongo, baada ya kufunga bao lake la kwanza kwenye mchezo dhidi ya Gwambina FC kwenye Uwanja wa Mkapa, Simba ikishinda 3-0.
Wawa ameeleza kuwa, ilikuwa ni siku ya furaha na historia kubwa baada ya kufunga bao hilo, kwani kwa kipindi chote alichocheza soka Tanzania, hakuwahi kufunga bao lolote na alisubiri siku hiyo kwa zaidi ya misimu minne na Mungu amejibu maombi yake kwa mara ya kwanza.
Wawa amesema: “Ilikuwa ni furaha kubwa sana kwangu kuweza kufunga bao langu la kwanza kwa ligi ya Tanzania, sijawahi kufunga kabla, hii ni mara yangu ya kwanza na nafikiri Mungu amejibu maombi yangu ya muda mrefu.
“Sasa naweza kuthubutu kusema, nitafanya jitihada hili niweze kufunga mabao mengi zaidi msimu huu, kama ambavyo wenzangu wanafanya, hiyo itakuwa bora kwangu na kwa timu. Mungu atanipa Neema.”
Wawa alitua Simba mwaka 2017 akitokea Al-Merikh ya Sudan, lakini kabla ya hapo alicheza Azam kwa misimu miwili 2014-16.
Jana Simba ilikuwa Dodoma ambapo ilicheza mchezo wake wa tano dhidi ya JKT Tanzania na kushinda kwa mabao 4-0. Leo kikosi kimewasili Bongo na mchezo wao unaofuata ni dhidi ya Yanga, Oktoba 18.
Kwa mabeki kinara wa kutupia ni Lamine Moro wa Yanga mwenye mabao mawili kibindoni.
Nakumbuka mechi inayofuat kabla ya Yanga kwa mujibu wa ratiba ni Prison au ratiba imebadilika?
ReplyDeleteMchezo dhidi ys Prisons umeahirishwa.
ReplyDelete