October 25, 2020

 


WAZIR Junior amesema kuwa ndoto yake ni kuwa mfungaji bora wa msimu wa 2020/21 baada ya kufunga bao moja kwenye ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya KMC leo Oktoba 25, Uwanja wa CCM Kirumba.


Yanga ilikuwa na kibarua cha kusaka pointi tatu mbele ya KMC na ilifanikiwa kufanya hivyo baada ya kupindua meza kibabe kwa kuwa ilianza kufungwa na wapinzani wake kipndi cha kwanza.

Dakika ya 26 Hassan Kabunda winga mzawa wa KMC alipachika bao moja kali akiwa nje ya 18 baada ya kujikunjua na kupiga shuti lililotibua rekodi ya clean sheet za Metacha Mnata ambaye alikuwa hajafungwa baada ya kukaa langoni kwenye mechi tano mfululizo za ligi.

Bao hilo liliwekwa sawa kwa mkwaju wa penalti na Tuisila Kisinda dakika ya 40 baada ya mwamuzi wa kati Ramadhan Kayoko kutafsri kuwa Michael Sarpong amechezewa faulo ndani ya 18.

Wazir Junior ambaye ameanza leo kwa mara ya kwanza kikosi cha kwanza alipachika bao lake la kwanza dakika ya 60 kwa pasi ya Farid Mussa na kutoa jezi kuonyesha maneno aliyoandika namna hii:" The King Of CCM Kirumba Stadium" na kwa kitendo hicho alionyeshwa kadi ya njano.

Wazir amesema kuwa :"Ndoto yangu ilikuwa ni kushinda, nimecheza mechi 60 za Ligi Kuu Bara na nimefunga mabao 34, kwa makipa wote ambao walikuwa wamewahi kusumbua ndani ya Bongo nilikuwa nimeshawafunga isipokuwa Juma Kaseja hivyo kumfunga leo kwangu ni furaha.

"Malengo yangu ni kuona kwamba ninaweza kuwa mfungaji bora na hilo linawezekana kwani msimu uliopita nilikuwa nafasi ya pili baada ya kufunga mabao 13 msimu huu malengo yangu ni kuwa mfungaji bora," amesema.

Ushindi huo unaifanya Yanga kuwa nafasi ya pili na pointi zake kibindoni ni 16 baada ya kucheza mechi saba na imeshinda mechi sita na ina sare moja.

Kinara ni Azam FC mwenye pointi 21 akiwa amecheza jumla ya mechi saba hajapoteza mchezo mpaka sasa.

2 COMMENTS:

  1. Ligi hii ni ngumu sana hakuna timu rahisi...unajua Simba au Yanga au Azam FC wanapokuwa wanafanya tambo nyingi kwenye magazeti na TV na kwenye radio pamoja na mashabiki wao wakijinasibu na kuwa mihemko kuwa watashinda mechi inayohusika hizi timu ndogo ndogo zinakuja zikiwa zimejipanga kwelikweli na kukamia 110% na matokeo yake hufanya mechi kuwa ngumu mno kwa Yanga na Simba ama Azam FC...lazima mashabiki wa timu kubwa waelewe hakuna timu itakuja uwanjani legelege kuja kuacha pointi ama kufungwa kizembe....kwahiyo kazi bado ni ngumu kwa Vigogo wa Ligi hii!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic