UONGOZI wa Simba umesema kuwa kesho utapambana kusaka pointi tatu kwenye mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Ruvu Shooting utakaochezwa Uwanja wa Uhuru.
Mchezo huo ni wa saba kwa Simba ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara ambao wapo nafasi ya nne kwenye msimamo na pointi zao kibindoni ni 13.
Inashuka uwanjani ikiwa na hasira za kuchezeshwa ligwaride na Tanzania Prisons, Oktoba 22, Uwanja wa Nelson Mandela kwa kufungwa bao 1-0 na kuwafanya waache pointi tatu mazima mbele ya Prisons, Rukwa.
Sven Vandenbroeck, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa kupoteza kwao mchezo wao mbele ya Prisons ni maumivu makubwa kwao lakini hakuna namna ya kufanya kwa kuwa ni sehemu ya matokeo ndani ya uwanja.
"Ni mchezo na tuliyopata ni matokeo, hivyo kwa sasa ambacho tunakifanya ni kujiweka sawa kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya Ruvu Shooting.
"Malengo yetu bado hayajabadilika kwani tunahitaji kupata pointi tatu muhimu ili kuweza kufikia malengo ambayo tumejiwekea ikiwa ni pamoja na kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara, mashabiki wajitokeze kwa wingi," amesema.
Simba nakutana na Ruvu Shooting ambayo imetoka kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na KMC Uwanja wa Uhuru.
Kwenye msimamo Ruvu Shooting ipo nafasi ya 10 kibindoni ina pointi zake tisa baada ya kucheza mechi saba za ligi.
Msimu uliopita mchezo wao wa mwisho kukutana Uwanja wa Mkapa ngoma ilikamilika kwa sare ya kufungana bao 1-1 hivyo kesho ngoma itakuwa nzito kwa pande zote mbili.
Ligi hii ni ngumu sana hakuna timu rahisi...unajua Simba au Yanga au Azam FC wanapokuwa wanafanya tambo nyingi kwenye magazeti na TV na kwenye radio pamoja na mashabiki wao wakijinasibu na kuwa mihemko kuwa watashinda mechi inayohusika hizi timu ndogo ndogo zinakuja zikiwa zimejipanga kwelikweli na kukamia 110% na matokeo yake hufanya mechi kuwa ngumu mno kwa Yanga na Simba ama Azam FC...lazima mashabiki wa timu kubwa waelewe hakuna timu itakuja uwanjani legelege kuja kuacha pointi ama kufungwa kizembe....kwahiyo kazi bado ni ngumu kwa Vigogo wa Ligi hii!
ReplyDeleteUko sahihi mkuu
Delete