October 9, 2020

 



HASSAN Bumbuli, Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa kikosi chao kipo tayari wakati wowote kucheza na Simba hata bila ya uwepo wa Kocha Mkuu ndani ya kikosi hicho na wanapata matokeo chanya.


Awali ilipaswa Yanga kukutana uwanjani na Simba inayonolewa na Sven Vandenbroeck, Oktoba 18 ila baada ya Bodi ya Ligi Tanzania, (TPLB) kuipeleka mbele mechi hiyo itachezwa Novemba 7.

Oktoba 7, TBLB iliweka wazi taarifa ya kupelekwa mbele mechi kwa sababu ilieleza kuwa uwepo wa uwezekano wa wachezaji wa timu hizo mbili walioitwa timu zao za Taifa kupata vikwazo kwenye masuala ya usafiri jambo litakaloathiri vikosi hivyo viwili.

Miongoni mwa wachezaji walioitwa kwenye timu zao za Taifa kwa Yanga ni pamoja na Metacha Mnata, Bakari Mwamnyeto huku kwa Simba ikiwa ni pamoja na Said Ndemla na Clatous Chama.

Bumbuli amesema:"Kwetu sisi Yanga huwa hatuihofii Simba wakati wowote tunaweza kucheza nao na tukapata matokeo chanya kwani tunajiamini.

"Hata sasa ukituambia kesho tunacheza na Simba ama baada ya kutoka pre season tuanze na Simba tunafanya hivyo. Hatuna kocha sawa, tunaweza kumpa timu shabiki na akakifundisha kikosi na kikacheza na Simba."

Msimu wa 2019/20, mchezo wa kwanza kuwakutanisha watani hawa, Januari 4, Simba ililazimishwa sare ya kufungana mabao 2-2, mchezo wa pili Yanga ilishinda bao 1-0, Machi 8.

2 COMMENTS:

  1. basi mumuache huyo huyo Mwambusi...ya nini kuleta kocha wa U20?
    Halafu hapa kila ukifungua Yanga mala wanesema hivi kuhusu mechi ya Simba...mpira huchezwa uwanjani...tulieni dawa itawaingia tu ili mseme refa alihongwa...mara kuna wachezaji wamehongwa...visingizio

    mmesikia mechi imesogezwa waliotegemea Miq hatacheza sasa yumo maana kabla ya Yanga kuna mechi ya kagera

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic