VINARA wa Ligi Kuu Bara, Azam FC tayari mapumziko yao ya siku mbili waliyopewa wamemaliza na wameshaanza maandalizi kwa ajili ya mechi zao za Ligi Kuu Bara pamoja na mechi za kirafiki.
Wakiwa nafasi ya kwanza baada ya kucheza mechi tano na kukusanya pointi 15 hawajapoteza mchezo hata mmoja mpaka sasa.
Oktoba 7 walianza mazoezi rasmi kwenye uwanja wao wa kimataifa wa Azam Complex. Mchezo wake unaofuata ndani ya ligi ni dhidi ya Mwadui FC.
Mchezo huo utachezwa Oktoba 15, Uwanja wa Azam Complex na Azam FC wakiwa ni wenyeji w mchezo huo. Awali ilipangwa kuchezwa Oktoba 9 ila mabadiliko ya Bodi ya Ligi Tanzania, (TPLB) yameupitia pia.
Mwadui imetoka kushinda bao 1-0 dhidi ya Namungo FC Kwenye mchezo wake wa raundi ya tano inakutana na Azam FC ambayo imetoka kushinda mabao 4-2 dhidi ya Kagera Sugar.
0 COMMENTS:
Post a Comment