UONGOZI wa Yanga umesema kuwa upo tayari kwa ajili ya mechi za ligi pamoja na nyingine zote bila kujali inakutana na nani ndani ya uwanja.
Jana, Yanga ilishinda bao 1-0 mbele ya Mwadui FC kwenye mchezo wa kirafiki uliochezwa Uwanja wa Azam Complex.
Bao pekee la ushindi lilifungwa na Michael Sarpong dakika ya 81 na kuwafanya mashabiki wa Yanga kusepa na furaha kwa ushindi kwenye mechi hiyo iliyokuwa na ushindani mkubwa.
Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya ushindani na wanatambua kwamba kila mechi ni ngumu na wapinzani wao wanakuwa wakiwakamia kupata ushindi.
"Kila mchezo kwetu ni mgumu kwa kuwa wapinzani wetu wanapambana ndani ya uwanja, kila timu ambayo inakuja uwanjani inatambua kwamba inakuja kupambana na timu kubwa.
"Kikubwa mashabiki wetu sapoti katika hili kwani kila mchezaji anatambua kwamba kwa sasa tunahitaji kushinda mechi zetu hivyo kikubwa tutazidi kupambana, tupo tayari," amesema.
Yanga ipo nafasi ya pili kwenye msimamo ikiwa na pointi 13 imecheza mechi tano imefunga mabao saba na kufungwa bao moja.
Nafasi ya 2 ????Jweli mahaba niue kwa makanjanja wa hili timu.
ReplyDeleteMnakamiwa kwa kipi mlichokuwanaco cha kutisha timu nyingi hata mkatisha? Si vibaya kujipa moyo
ReplyDeleteAcheni uzushi mabingwa watetezi wasemeje sasa nyie hata konbe la mbuzi hamna
ReplyDeleteMahaba niue mnawapandisha nafasi kinguvu
ReplyDeleteHivi utopolo mnajiona kuwa timu bora hako kausajili ndio kanakowadanganya.Mjue kabisa hakuna timu lainilaini kama mnavyofikiria labda mimi naona uto ndio timu lainilaini. Ligi ndio kwanza mbichi mnalalamika duuu amueleweki hakuna pointi za mezani subirini mkutane na mnyama ndio mtajua cha moto.
ReplyDeleteUtopolo wanajitia moyo kifo kinawanyemelea na hakikimbiiki
ReplyDeleteHuu sasa utoto, ndio inashinda kwa kubahatisha na inacheza mpira mbovu nani awakamie hao jamani
ReplyDeleteZlatko alijitetea timu haina muunganiko, akafanikiwa kuwaaminisha kuwa timu haina muunganiko kumbe anaficha mapungufu yake ya kimbinu SASA na Mwambusi ameanzisha kisingizio kuwa timu inakamiwa, Yanga inakamiwaje? Mwadui wamemiliki mpira asilimia 60 Yanga asilimia 40 !! Halafu unasema Yanga inakamiwa? Wachezaji hawajui kuanzisha mpira kunyang'anya mipira kumiliki mpira unasema wanakamiwa? Yanga waishukuru TFF na serikali maana oktoba 18 wangefungwa si chini ya goli 8 na pengine uchaguzi usingekwenda vizuri, ndio maana uchaguzi umeachwa upite ili mechi ifuate baadae ili kutowavuruga kisaikolojia wapiga kura.
ReplyDeleteNyie wote si mmenunuliwa na MO ndio mnafurahi
ReplyDeletePanzi kweli
Delete