KLABU ya Yanga imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mwadui FC kwenye mchezo wa kirafiki uliochezwa Uwanja wa Azam Complex.
Bao la ushindi kwa Yanga limefungwa na mshambuliaji wao namba moja Michael Srpong dakika ya 81 na kuwainua mashabiki wa timu ya Yanga inayonolewa na Kaimu Kocha, Juma Mwambusi.
Huu ni mchezo wa kwanza kwa Mwambusi kusisimama akiwa kwenye benchi baada ya Zlatko Krmpotic kufutwa kazi Oktoba 3 baada ya kumaliza mchezo wake wa mwisho dhidi ya Coatal Union, Uwanja wa Mkapa.
Ushindani ulikuwa ni mkubwa kwa timu zote mbili ambapo umakini kwa washambuliaji wa Mwadui pamoja na Yanga uliwafanya wakamilishe dakika 45 za mwanzo bila kufungana.
Wazir Junior wa Yanga alikosa nafasi mbili za wazi ambazo angekuwa makini angeweza kufunga mabao kwa timu yake ila alipiga mashuti ambayo hayakulenga lango.
Mimi nilitaraji timu yangu itaondoka na ushindi mnono kutokana na ubora wa timu yetu na kiwango cha Mwadui tukionacho Katika mechi za ligi na pia baada ya kutimuliwa Msarbia, inavosemekana kutokana na udhaifu wake
ReplyDeleteWewe unatarajia matokeo tu hakuna kitu kingine, duuuh!
DeleteTeam inajengwa bdo mafundi hawajamaliza kz
ReplyDeleteKwa kiwango kipi?Tunabebwa na magazeti uchwara na blogu vipofu.
ReplyDeleteTimu inaonyesha kiwango dhaifu. Tumefukuza kocha sioni kosa lake. Wachezaji ni majina tu na kama kocha amefukuzwa kwa wao kulalamika basi tuna safari ndefu sana.
Ni maoni yako
DeleteUnajiita Yanga damu kitu gani, mashabiki maandazi kama nyie ndio mnaoifikisha hapa Yanga ilipo, watu wanao ikosoa Yanga sio wote ni simba tunaikosoa kwakuwa tunataka iwe bora, timu mbovu unataka tusifie timu mbovu, mwanzo tulisema zlatko hafai wapo mashabiki maandazi kama wewe walimtetea mwishowe ukweli ukawa wazi akaonekana hafai na kwa taarifa yako Simba walitamani Zlatko na Mwambusi wawepo tarehe 18. chunguza kwa umakini utagundua simba wameumia sana zlatko kuondolewa Yanga na hawapendi Kaze aje Yanga kwakuwa wanajua atawasumbua, hivi sasa kuna kampeni chini kwa chini simba wanataka Mwambusi asimame kwenye benchi nov 7, udhaifu wa kocha ndio udhaifu wa timu uwanjani, kocha lazima awajibike kama timu haipafomu vizuri.
DeleteJUMA MWAMBUSI NI TATIZO KUBWA LA YANGA LILILOBAKIA, BAADA YA KUONDOKA KWA ZLATKO. CEDRIC KAZE AJE NA MSAIDIZI WAKE HUYU MWAMBUSI HAJITAMBUI.
ReplyDeleteTanzania wachambuzi wa soka ni wengi kupita maelezo!
DeleteMimi sio Yanga bendera kufuata upepo. Kiwango hakiridhishi. Ukweli lazima usemwe.
ReplyDeleteKama mnaona gari lina enda pole pole, teremkeni msubiri lingine Sio lazima hili tuu
ReplyDeleteUkifukuza kocha, vunja benchi nzima na unda jipya na sivyo yatakuwa yaleyale tu
ReplyDeleteSiyo kuwa yatakuwa yaleyale, lakini kwa jinsi nilivowona mchezo ndio yameshakuwa. Kwa mpira Wa ufundi na busara Costal walikuwa bora na kwa upande wa maguvu na mabavu, upande wa pili tuwape haki yao.
ReplyDeleteTimu inajengwa bado kwahivo tungoje inyeshe mvuwa ndipo tuzione radi za Kagere, Chama Konde boy na wengineo ndipo tutapouona umadhubuti wake
ReplyDeleteHivi kwa wachezaji wa kigeni wa Yanga nani anachezea team ya taifa?
ReplyDeleteWote viwango huko kwao havikidhi haja na ndio wametapeli babu jinga kila mmoja kachukuwa chake. Mbona wenye mana wa Azam na Simba wamechukuliwa
ReplyDeleteUKIKOSA HELA UNA KOSA MPAKA UFAHAMU WA MAMBO. YANGA TATIZO NI HELA, WADHAMINI HAWANA HELA VIONGOZI HAWANA HELA NA MASHABIKI HAWANA HELA. TUNAISHIA KULALAMA NA KUONGEA ONGEA HOVYO, TATIZO RASILIMALI FEDHA, MASKINI SIKU ZOTE NI MUONGEAJI SANA, TAJIRI KWAKE NI VITENDO TU. YANGA MANENO MEEEEENGI KAMA BENDI YA MIPASHO AU TAARABU. TUBADILIKE KUANZIA MASHABIKI, VIONGOZI NA WADHAMINI.
ReplyDeleteIvi simba na yanga wamepshana point ngap?
ReplyDelete