BEKI wa Arsenal Gabriel
Magalhaes amesema kuwa amekuwa
akimkubali sana beki Virgil van Dijk anatamani kucheza dhidi yake pamoja na Sergio Aguero.
Gabriel amesajiliwa na Arsenal msimu huu akitokea katika Klabu ya Lille ya Ufaransa kwa kiasi cha pauni 27m.
Gabriel amesema:“Katika mabeki ambao ni
nawakubali sana ni Van Dijk na
nimefurahi nimecheza dhidi yake jambo ni
changamoto kwangu pia.
“Pia
nimecheza dhidi ya Man City japo tulipoteza ila tulijifunza mengi kutoka kwao. Nikacheza dhidi ya mchezaji bora Aguero ambaye mabeki wengi
wanatamani kucheza naye na kujua ni staili ipi wanaweza kucheza naye.
“Tumeshacheza
na timu kubwa na tumejifunza mengi na
kuangalia wapi tunatakiwa kufanya marekebisho hasa tunapokuwa uwanjani.
“Lakini kwa ujumla ligi hii ina ushindani sana kuliko kawaida na ndiyo
maana nilichagua kuja Premier League.
Hata hivyo, Gabriel alieleza kuwa wakati anakipiga katika Ligue
1 straika ambaye alikuwa akimsumbua zaidi
alikuwa ni Kylian Mbappe wa PSG.
0 COMMENTS:
Post a Comment