LIGI Kuu Tanzania Bara inatarajia kuendelea kutimua vumbi jioni ya leo kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.
Tangu Ihefu ipande leo hii ndiyo
inaingia kwenye dabi kati yake na Mbeya City kabla ya kuwavaa Prisons mchezo
unaofuata.
Akizungumzia maandalizi kuelekea
mchezo huo Kocha Mkuu wa Ihefu, Zubeir Katwila, amesema wamejiandaa vizuri
kuhakikisha wanapata pointi tatu kwenye mchezo huo.
"Tumejiandaa vizuri kuwakabili
ndugu zetu na tunaimani tutapata matokeo chanya na kuondoka kwenye nafasi ya
mwisho katika msimamo," amesema.
Kwa upande wake kocha msaidizi wa
Mbeya City, Mathias Wandiba yeye ametamba kuendeleza wimbi la ushindi kwenye
mchezo huo.
"Maandalizi yamekamilika na
wachezaji wako kwenye hali nzuri na morali iko juu kuelekea mchezo huo ambao
utakuwa mgumu lakini imani yetu nikuwa tutashinda," amesema .
Mbeya City inaingia uwanjani ikiwa na kumbukumbu ya kushinda mabao 2-1 dhidi ya Kagera Sugar, Uwanja wa Kaitaba.
0 COMMENTS:
Post a Comment