November 29, 2020


 BAADA ya kufungua rasmi akaunti yake ya mabao ndani Ligi Kuu Bara akiwa na kikosi cha Klabu ya Simba kwenye mchezo wa Jumamosi dhidi ya Coastal Union, kiungo mshambuliaji wa Simba raia wa Ghana, Bernard Morrison ametamba kuwa sasa gari limewaka na anaamini moto huo ataendelea nao kwenye michezo ya kimataifa.

 

Simba ipoNigeria kwa sasa ikiwa kwenye maandalizi ya mwisho kujiwinda na mchezo wake wa kwanza kwenye michuano ya klabu bingwa Afrika dhidi ya Plateau United ya Nigeria, unaotarajiwa kupigwa kati ya Novemba 27 hadi 29 mwaka huu.

 

Morrison aliyetambulishwa rasmi kuwa mchezaji wa Simba Agosti 8, mwaka huu alikuwa kwenye wakati mgumu tangu msimu huu ulipoanza, ambapo kabla ya mchezo huo wa Jumamosi alikuwa tayari amecheza michezo nane bila kuona nyavu za wapinzani.

 

Simba Jumamosi iliyopita iliibuka na ushindi wa mabao 7-0 huku Mghana huyo akihusika kwenye mabao mawili baada ya kufunga bao moja na kuasisti bao moja lililofungwa na nahodha wa Simba, John Bocco ambaye alifunga mabao matatu ‘Hat-trick’ kwenye mchezo huo.

 


Morrison amesema:-“Kwa upande wangu nashukuru Mungu kwa sababu nimefanikiwa kufunga bao langu la kwanza nikiwa na Simba msimu huu.

 

“Ni matumaini yangu kuwa nitaendeleza moto huu kwa kuhakikisha ninafunga mabao mengi zaidi, kwa ajili ya kuisaidia Simba kufikia malengo tuliyojiwekea kwenye ligi na hata kwenye michuano ya klabu bingwa Afrika,”

 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic