November 29, 2020


 AZAM FC kesho itakuwa Uwanja wa Karume, Mara kusaka pointi tatu mbele ya Biashara United.


Ikiwa chini ya kocha msaidizi, Vivier Bahati ambaye amepewa mechi mbili ataanza kumaliza dakika zake 90 kesho kabla ya kumaliza na Gwambina FC.


Bahati amepewa mechi hizo baada ya Aristica Cioaba kufutwa kazi Novemba 26 kutokana na kile kilichoelezwa matokeo mabovu ndani ya timu.


Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Azam FC Zakaria Thabit amesema kuwa maandalizi yapo sawa na kila mmoja yupo tayari kusaka pointi tatu muhimu.


"Tupo tayari kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya Biashara United ni matumaini yetu kwamba tutafanya vizuri na kupata pointi tatu ili turejee kwenye ubora wetu," amesema.


Azam FC inashuka uwanjani ikiwa na kumbukumbu ya kupoteza mechi mbili mfululizo, ilianza kupoteza mbele ya KMC kwa kufungwa bao 1-0 Uwanja wa Uhuru na ikapoteza mbele ya Yanga kwa kufunga bao 1-0 Uwanja wa Azam Complex.


Kwenye msimamo ipo nafasi ya pili baada ya kucheza mechi 12 imekusanya jumla ya pointi 25 kibindoni.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic