November 9, 2020

 


BIGIRIMANA Blaise mtupiaji namba moja ndani ya Klabu ya Namungo FC amesema kuwa kikubwa kinachompa nguvu ya kufanya vizuri ni Mungu pamoja na juhudi ndani ya uwanja.


Namungo kwenye msimamo ipo nafasi ya 8 imekusanya pointi 14 baada ya kucheza mechi 10 ndani ya Ligi Kuu Bara.


Imefunga jumla ya mabao saba na kinara wa utupiaji Blaise ametupia mabao manne na ni mshambuliaji wa kwanza ndani ya ligi kufunga bao msimu wa 2020/21 alipofunga bao hilo mbele ya Coastal Union, Uwanja wa Majaliwa kwa pasi ya kipa Nurdin Barola.


Akizungumza na Saleh Jembe, Blaise amesema:"Ni Mungu ananipigania kwani kabla ya mechi kuanza na baada ya kumaliza kitu cha muhimu kwangu ni kuomba ili anipe nguvu ya kufanya vizuri zaidi.


"Ushindani ni mkubwa na kila mchezaji anahitaji kufanya vizuri kwa ajili ya timu, kwangu mimi naanza na timu kisha nafasi yangu ya kufunga baadaye." 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic