November 9, 2020

 


DABI ya Kariakoo kwa misimu miwili imegubikwa na maamuzi tata kuhusu penalti kwenye mechi zote mbili za mzunguko wa kwanza.

Novemba 7, Uwanja wa Mkapa licha ya kuwepo jumla ya waamuzi sita ambapo mmoja alikuwa ni wa kati ambaye ni Abdalah Mwinyimkuu pamoja na waamuzi wengine wawili waliokuwa pembeni ya magoli pamoja na wale wawili washika vibendera bado walianguka kwenye mtengo wa msimu uliopita.

Kwenye mchezo huo ambao ulishuhudia dakika 90 ngoma ikikamilika kwa sare ya kufungana bao 1-1, bao la kwanza la Yanga lilifungwa na Michael Sarpong kwa  mkwaju wa penalti baada ya Joash Onyango beki wa Simba kuonekana akimchezea faulo Tuisila Kisinda nje kidogo ya 18 na likafunikwa tuta.

Ikumbukwe pia, Januari 4,2019 Uwanja wa Mkapa licha ya uwepo wa waamuzi sita na mwamuzi wa kati kuwa ni Jonesia Rukya alitoa penalti kwa Simba iliyofungwa na Meddie Kagere ambaye alionekana kuchezewa faulo na Kelvin Yondani nje kidogo ya 18.

Kwenye dabi hiyo ya mzunguko wa kwanza ngoma ilikamilika 2-2 na baada ya mchezo huo waamuzi hao ikiwa ni pamoja na Jonesia walipewa onyo na Shirikisho la Soka Tanzania,(TFF) kwa kushindwa kutafsiri sheria 17 za mpira.

 Mwenyekiti wa Kamati ya Waamuzi Tanzania, Soud Abdi Mohamed amesema kuwa jopo la wataalamu wa masuala ya waamuzi litakaa kujadili na kupitia masuala yote ambayo yametokea kwenye mechi za ligi ikiwa ni pamoja na mchezo wa dabi.

4 COMMENTS:

  1. Hilo limepita, aliyepata kapata, aliyekosa asubiri zamu yake, ndio kpira wetu huu

    ReplyDelete
  2. hata kama zote ni nje umbali wa nje ya juzi umezidi..ya juzi ilikuwa nje zaidi..pia Jonesia hakuwanyima Yanga penalti halali..Refa wa juzi alikuwa na matokea yake mfukoni mara nne faulo za deadball zinazoanzia kati Simba wakianzisha anadai apulize kwanza filimbi...filimbi husubiriwa ikiwa ni eneo hatari...sio watu wanapanga shambulizi halafu refa anavuruga..sio penal5i tu kuna matukio mengi tata zikiwemo kadi tatu za Simba wakati Yanga wao wanacheza faulo wanavyotaka..atakuwa aliumia sana Simba iliposawazisha dak 85

    ReplyDelete
    Replies
    1. Aahaaaaaaa jmn kweli mpira hatuujui tukae tu kimya zote nje ila nyingine ni mbali

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic