November 13, 2020

 


BAADA ya Novemba 11, 2020, mshauri wa Klabu ya Yanga SC, Senzo Mazingisa, kuhojiwa na maofisa wa Polisi katika kituo cha Polisi cha Oyster Bay kwa masaa yasiyopungua matatu kisha kuachiwa huru, mtaalamu huyo wa masuala ya uongozi wa soka ametoa neno kwa wadau wa soka.

 

Senzo kupitia ukurasa wake rasmi wa mtandao wa kijamii wa Instagram (football_Senzo) aliandika maneno haya; “Mpira wa miguu hautalala kamwe, Sijawahi kugundua kuwa kuhama kutoka Simba kwenda Yanga kunanisababishia uhasama mwingi kiasi hiki.

 

“Sasa ni dhahiri kwamba nimesababisha kuumizwa na chuki katika undugu wa mpira wa miguu wa Tanzania kwa kiwango ambacho watu watahatarisha yote kuchafua jina langu kwa kutaka kulipiza kisasi. Niko salama na mzima, niko nyumbani na ninatarajia kutumika. Asante wananchi wenzangu, tuko pamoja,” aliandika Senzo.

 

Taarifa za mitandao mbalimbali zinadai sababu za Senzo kuhojiwa ni kuwepo na tuhuma za mawasiliano yake na aliyekuwa Mkurugenzi wa Wanachama kwenye Klabu ya Simba, Hashim Mbaga.

 

Senzo aliwahi kuwa Mtendaji Mkuu wa Simba ambapo alijiuzulu nafasi hiyo na kwenda kuajiriwa na Yanga ambao ni mahasimu wakubwa wa Simba.

 

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Yanga, Hersi Said, amejibu kuhusu sakata hilo akiandika kuwa limefikia sehemu ambayo siyo utani tena bali uadui akidai utani umeishia uwanjani.


Pia Uongozi wa Yanga ulitoa taarifa kwamba umesikitishwa na kushikiliwa kwa kiongozi huyo na kuhojiwa kuhusu ishu za kupanga matokeo na kupinga propaganda zisizo za kiungwana.

4 COMMENTS:

  1. Umbea wake ndo umemponza na utamponza zaidi tu. Afanye kazi kiuprofesional aache umbea utopolo alioambukizwa utamponza na CV yake anazidi kuichafua.

    ReplyDelete
  2. Shame on u. Simba ndio mnajidhalilisha kwa tuhuma za kitoto kisa tu katoka simba. Hivi nyie msifungwe mmekua nani? Simba ni timu ya kawaida kama nyingine kujaza wahindi sio kwamba inatoka india

    ReplyDelete
    Replies
    1. 😄😄👆 unanifurahisha kwelikweli, subiri polisi wafanye Yao kwanza umbea utamtokea puani.

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic