November 6, 2020


 MAMBO ni mazito kwa mabingwa watetezi Simba ambao kesho wanakutana na Yanga kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa Uwanja wa Mkapa na huenda kesho wakakosa jumla huduma ya mtambo wao wa mabao Clatous Chama.


Simba ikiwa imefunga mabao 21 Chama amehusika kwenye mabao saba ambapo ametoa pasi tano za mabao na kutupia mabao mawili.


Kwenye mechi mbili ambazo hakuwepo kikosi cha kwanza wala benchi, Simba iliambulia maumivu kwa kupoteza pointi sita na kufungwa jumla ya mabao mawili ndani ya dakika 180.


Ilifungwa bao 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons Uwanja wa Nelson Mandela na ikachapwa bao 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting Uwanja wa Uhuru.


Kwa mujibu wa Sven Vandenbroeck, Kocha Mkuu wa Simba, amesema kuwa maandalizi yapo sawa ila atakosa huduma ya Chama kwa kuwa ni majeruhi.


Kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Kagera Sugar Chama hakumaliza dakika 90 alitoka na kumpisha Miraj Athuman dakika ya 69.

9 COMMENTS:

  1. Replies
    1. Chanzo ni YouTube kwa hisani ya VPN😁😁😁😁

      Delete
  2. Sio kweli nimeongea na mtu wa karibu na uongozi.

    ReplyDelete
  3. Mmiliki wa hii blog ni typical Yanga,anapambana sana kutuharibu kisaikolojia.

    ReplyDelete
  4. Utopolooo! Kesho Kuna sapraiz according to kaduguda. Utopolo wacha walewe misifa kesho mapemaaa watalala na viatu na kuamka saa sita mchana aibuuu.

    ReplyDelete
  5. Nguruwe fc tulia dawa ikuingie vizuri,pale bila Chama lazima mliwe kiboya sana, na hata angekuwemo ni kumkaba mpka akafanyiwa substitution manyumbu fc nyie

    ReplyDelete
  6. Hiyo Ni Mbinu Ya Kivita Tunata Utopolo Waje Kwa Wingi Then Mara Paaa Suprise Chama Ndani Tuwareee

    ReplyDelete
  7. Habari ya kuizuga Yanga; Awepo Chama au asiwepo kichapo kiko palepale

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic