November 29, 2020


 JONNY Evans, nyota wa zamani wa Klabu ya Manchester United anatajwa kuwekwa kwenye rada na mabosi wake hao ambao wapo kwenye mpango wa kumrejesha kundini msimu ujao.


Nyota huyo ambaye kwa sasa anakipiga ndani ya Leicester City mkataba wake unafika ukingoni msimu ujao jambo ambalo linaipa nafasi Manchester United kuipigia hesabu saini yake.


Beki huyo raia wa Ireland Kaskazini alicheza jumla ya mechi 198 alipokuwa kwenye academi ya Manchester United na aliweza kushinda jumla ya mataji matatu ya Ligi Kuu England kabla ya kuibukia West Brom msimu wa 2015.


United imeona kwamba uwezo wake ndani ya Leicester City ni mkubwa jambo lililowavutia United chini ya Kocha Mkuu Ole Gunner Solskjaer kwa mujibu wa the Sun.


Evans amepewa dili jipya la kusaini ndani ya Leicester City ambapo mpaka sasa bado hajasaini licha ya kuweka wazi kuwa anafurahia maisha ya hapo.


"Ninafurahia sana maisha ya hapa," amesema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic