November 29, 2020

 


MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu England jana Novemba 28 walibanwa mbavu mbele ya Brighton wakati wakilazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na kupunguziwa kasi ya kuteta ubingwa wao wakiwa ugenini.


Nyota Diogo Jota alizidi kuwaka baada ya kupachika bao la kuongoza dakika ya 60 na ndani ya dakika za nyongeza Danny Welbeck  nyota wa Liverool alifanya madhambi ambapo kwa msaada wa VAR mwamuzi aliamuru ipigwe penalti na mpigaji alikuwa ni Pascal Gross ambaye aliijaza kimiani.

Mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Falmer ilibaki kidogo kikosi cha Liverpool kipoteze mazima pointi tatu baada ya Brighton kupata penalti kipindi cha kwanza iliyokoswa na Neal Maupay na kitendo hicho kilimfanya kocha wake amtoe uwanjani. 


Hii no sare ya tatu kwa Liverpool msimu huu lakini Brighton wanaonekana kupata sare nne ipo nafasi 16 na pointi zake ni 10 na Liverpool imecheza jumla ya mechi 10 ina pointi 21 ikiwa nafasi ya kwanza.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic