IMEFAHAMIKA kuwa kiungo mchezeshaji raia wa Zambia, Clatous Chama, amekataa mkataba wa miaka miwili Simba wenye dau la Sh milioni 150 huku watani wao wa jadi wakimtengea Sh milioni 300.
Kiungo huyo fundi, hivi karibuni ilielezwa amegomea mkataba wa miaka miwili wa kuendelea kuichezea Simba huku akiwataka viongozi kusubiria hadi mkataba wake utakapomalizika mwishoni mwa msimu huu.
Yanga hivi karibuni ilielezwa imeanza mazungumzo ya siri na meneja wa kiungo huyo kwa ajili ya kuhitaji huduma yake msimu ujao baada ya mkataba wake kumalizika Simba.
Taarifa zinaeleza kuwa Yanga imerejea kimyakimya kwa meneja wa kiungo huyo kwa ajili ya kuanza mazungumzo ya awali ili wafanikishe mipango yao ya kumsajili Chama ambaye ni tegemeo hivi sasa kwenye kikosi cha Mbelgiji, Sven Vandenbroeck.
Mtoa taarifa amesema kuwa kiungo huyo kabla ya mchezo wa Dar es Salaam Dabi, alifanya kikao na Mwenyekiti wa Bodi ya Klabu ya Simba, Mohammed Dewji ‘Mo’ kwa ajili ya kufanya mazungumzo ya mwisho ya kukamilisha dili hilo la usajili.
Aliongeza kuwa mabosi wa Simba wamemuwekea kitita cha Sh 150Mil ambacho alitengewa ili asaini na kugoma huku akiomba kuongeza mkataba huo mwishoni mwa msimu.
“Vita kubwa ipo ya kimyakimya kati ya vigogo wa Simba na Yanga ambao wote wanawania saini ya Chama katika msimu ujao, licha ya kuwepo taarifa za kukanusha kuwa nyota huyo anaendelea kubakia Msimbazi.
“Siku moja kabla ya mchezo Dar es Salaam Dabi viongozi wa Simba walifanya kikao na Chama, katika kikao hicho viongozi hao wameonekana kumshawishi kiungo huyo asaini mkataba wa miaka miwili kwa dau la Sh milioni 150.
“Wakati Simba wakitaja dau hilo, Yanga wenyewe wanafanya mipango yao kimyakimya ambao wenyewe wapo tayari kumpa Sh milioni 300 ili asaini mkataba wa miaka miwili Jangwani,” alisema mtoa taarifa huyo.
Chama alilaumiwa na mashabiki wengi wa Simba kwa kucheza chini ya kiwango katika pambano dhidi ya Yanga Novemba 7.
Mjumbe wa Kamati ya Usajili na Mashindano wa Yanga ambaye pia ni Mkurugenzi wa Uwekezaji wa GSM, Injinia Hersi Said hivi karibuni alisikika akisema: “Kama uongozi tupo tayari kusajili mchezaji yeyote atakayependekezwa na kocha.
“Kikubwa hatutaki kumuingilia kocha wetu katika masuala yote yanayohusiana na usajili, hakuna mchezaji tutakayeshindwa kumsajili katika kuelekea usajili wa dirisha dogo.”
Ofisa Habari wa Simba amesema kuwa hakuna suala la Chama kutakiwa na timu yoyote kwa sasa akili zao wanaziweka kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.
Kwa sasa Chama yupo nchini Zambia ambapo amekwenda kwa ajili ya kuitumikia timu ya Taifa ya Zambia maarufu kama Chipolopolo ambayo itacheza leo dhidi ya Botswana.
Kocha yupi wa pasi fupifupi au ndefu ndefu au kupaki Basi
ReplyDeleteMwandishi siku moja kabla ya derby CHAMA alikua kambini,hicho kikao alifanya saa ngapi na viongozi wa YANGA?
ReplyDeleteSoma vizuri habari ngo'ombe wewe hajasema kafanya kikao na viongozi wa yanga kasemea kafanya kikao na viongozi wa mikia
ReplyDelete😆😆😆 utopolo hamjui psychology mwisho wa siku mtaishia kutama mbele ya viongozi,wanachama na mashabiki wa Simba mabingwa wanchi. *Juzi tu makam wetu katika kuchutama kwa viongozi na mashabiki wa Simba kwa hii ishu ya Chama* Simba hufanya kweli tuliongea kwa morsoni tukamchukua kweli utopolo mmedata ninyi kwa chama mwakalebela kachutama bonge la aibu. Ndo maana TFF alitimuliwa.
ReplyDeleteJuzi tu makam wenu mwakalebela kachutama kwa viongozi na wanachama wa Simba na ingwa wa nchi
ReplyDelete