November 11, 2020


TIMU ya Taifa ya Tanzania, chini ya miaka 20 leo Novemba 11 imekubali kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya timu ya Taifa ya Sudan.


Mchezo wa leo wa kirafiki umechezwa Uwanja wa Uhuru ambapo Sudan ilianza kufunga bao la kwanza dakika ya 10 kupitia kwa Mustafa Hassan dakika ya 10 na lile la pili lilifungwa na Nagigouma Alamin dakika ya 56.


Bao la kufutia machozi kwa Tanzania lilifungwa na Tepsi Evans dakika ya 63 na lilidumu mpaka dakika 90 zilipokamilika.

Nahodha wa timu ya Tanzania, Kelvin John amesema kuwa wameshindwa kutumia nafasi ambazo wamezipata jambo ambalo limewaadhibu.


"Ulikuwa mchezo mzuri na wenye ushindani, wenzetu wametumia makosa yetu kutuadhibu nasi tumeshinwa hivyo nina amini kwamba benchi la ufundi limeona makosa yetu litafanyia kazi," amesema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic