November 26, 2020


 JAMHURI Kihwelo,’Julio’ Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania, chini ya miaka 20, ‘Ngorongoro Heroes’ amesema kuwa wanaamini watapata ushindi leo mbele ya Somalia kwenye mchezo wa pili wa mashindano ya  CECAFA.

Mashindano hayo yanayofanyika mkoani Arusha,Karatu  na Tanzania ni wenyeji leo watakuwa na kibarua cha kusaka ushindi mbele ya Somalia ambayo imetoka kupoteza kwa kufungwa mabao 2-1 na Djibout kwenye mchezo uliochezwa Novemba 24, Uwanja wa Black Rhino Academy.

Ngorongoro Heroes kwenye mchezo wao wa ufunguzi uliochezwa Novemba 22, dhidi ya Djibouti, Ngorongoro Heroes waliibuka na ushindi wa mabao 6-1 huku Abdul Hamis akiweka rekodi ya kufunga hat trick na kusepa na mpira wake kwenye mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Black Rhino Academy, Karatu.

 

Julio amesema kuwa kila timu imejipanga kupata matokeo mazuri ndani ya uwanja  jambo ambalo wao wanalifanya hivyo wanaamini kwamba watapambana kupata ushindi kwenye mchezo huo.


”Kila timu ipo tayari kwa ushindani hilo linatupa nguvu nasi pia kuingia kutafuta ushindi, nimewaona vijana wana morali na nguvu ya kusaka ushindi hivyo imani yetu ni kwamba hatutawaangusha Watanzania tutapambana kupata matokeo.


"Timu ambazo zinashiriki nimeziona na zinafanya vizuri, vijana wetu wapo tayari na wanafurahi kuona kwamba wanapeperusha bendera ya Tanzania hivyo watafanya vizuri, kikubwa sapoti," . 


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic