November 12, 2020


MUSSA Mbissa, kipa namba moja wa Klabu ya Mwadui FC inayonolewa na Kocha Mkuu, Khaleed Adam ameweka rekodi yake ya kuwa kipa namba moja aliyefungwa mabao mengi kwa msimu wa 2020/21.


Akiwa kwenye majukumu ya kusaka pointi tatu, Adam amempa majukumu ya kuwa kipa kwenye mechi zake zote 10 ambazo ni dakika 900 na ameokota jumla ya mabao 20.


Ana wastani wa kuokota bao moja kila baada ya dakika 45 na timu yake ipo nafasi ya 15, imekusanya pointi 10 na safu ya ushambuliaji imefunga jumla ya mabao 8 na mechi ambazo alifungwa mabao mengi ilikuwa dhidi ya JKT Tanzania alipookota mabao 6-1 pamoja na mchezo dhidi ya Simba alipookota mabao 5-0.


Timu ambayo inafuata kwa kufungwa mabao mengi ni Kagera Sugar ambayo ipo chini ya Kocha Mkuu, Mecky Maxime ambayo imefungwa mabao 13 na Yanga inashika nafasi ya kwanza kwa timu ambazo zimefungwa mabao machache ambayo ni matatu ipo nafasi ya pili na pointi zake 24.


Kocha Adam amesema kuwa mpango mkubwa wa timu kwa sasa ni kufanyia kazi makosa yaliyopita ili kuwa bora kwa wakati ujao.


"Hakuna mwalimu anayepeleka timu uwanjani akifikiria kufungwa hivyo kupoteza kwetu ni somo kwa ajili ya mechi zetu zijazo," .


Novemba 22 itakuwa na mchezo dhidi ya Kagera Sugar, Uwanja wa Kaitaba saa 10:00 jioni.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic