November 12, 2020


 UONGOZI wa Yanga umesema kuwa suala la wachezaji wake wawili wazawa kudaiwa kuwa wanawaniwa na Klabu ya TP Mazembe linawapa matumaini ya kuamini kwamba timu yao inafuatiliwa na watu wengi duniani.


Feisal Salum pamoja na Bakari Mwamnyeto ambao wapo kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars kitakachocheza kesho, Novemba 13 dhidi ya Tunisia kwenye mchezo wa kuwania kufuzu Afcon 2021 nchini Cameroon wamekuwa wakitajwa kuingia anga za TP Mazembe ya Congo.


Nyota hao wamekuwa kwenye ubora wao kwa msimu wa 2020/21 ndani ya Ligi Kuu Bara wakiwa na uhakika wa kuanza kikosi cha kwanza kinachonolewa na Cedric Kaze.


Mwamnyeto ambaye ni beki ameshuhudia mabao matatu yakitikisa nyavu za timu yake kwenye mechi 10 ikiwa ni timu iliyofungwa mabao machache ndani ya ligi.


Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela amesema kuwa hawashangazwi na taarifa hizo kwa kuwa wachezaji wao ni bora na wana uwezo mkubwa.


"Ipo wazi kwamba tuna kikosi kizuri na chenye wachezaji makini hivyo wachezaji wetu kutakiwa na TP Mazembe naona sio jambo mbaya hivyo ofa ikija mezani basi tutajua tutafanyaje, na hii inamaanisha kwamba kikosi chetu kinafuatiliwa duniani" amesema. 

7 COMMENTS:

  1. Nyinyi wambieni kwa kila mchezaji shilingi milioni Mia tano na yule Shuwa Boy wa Azam mutoe ofa yenu ya milioni 35

    ReplyDelete
  2. Kama wanatakiwa nje basi Ni fresh hyo ndo maendeleo ya soka, lkn ctoshangaa nilisikia utopolo wamewazuia kuwatoa maana ndo ulimukeni wao toka enzi na enzi, baadhi ya viongozi wao bdo mambumbu sana kwenye,soka la biashara.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Umesikia wapi? x2

      Delete
    2. 😄😄😄 hufutiliagi mpira ww au ulikuwa bdo mtoto. Ngasa mmlimnyina fursa Mara ngapi kwenda nje ya bongo. Conveinger ya Canada alikokuwa Nuzar Khalifan, alinyimwa nafac ya kwenda Norway kwa Henhry Joseph Shindika na fursa nyingine nyingi tu kwasababu ya ulimbukeni wa utopolo viongozi na mashabiki wao

      Delete
  3. Ni kiongozi gani wa TP mazembe aliyesikika akisema,au ni gazeti gani limetoa hizo taarifa,shida ya hii blog ni source of information.Ni jambo la heri kama iko hivyo maana tutakuwa na timu ya taifa nzuri,lakini hakuna chanzo cha taarifa,je ni mawakala wa wachezaji,kiongozi wa yanga au Tp mazembe au magazeti ya kongo?Mwakalebela kwa kauli yake hapo juu nayeye kama anazisikia ila hashangazwi.

    ReplyDelete
  4. Bora uandike hivi wachezaji wapate moyo kwa kucheza kwa kujituma na sio kubebwa na marefa

    ReplyDelete
  5. Huu mpira wa kuujulia uzeeni ni shidaa.Kipi cha ajaabu Kwa wachezaji hao kwenda TP Mazembe?wakati kuna wachezaji wengine wa kitanzania kina Ulimwengu, Singano na Ambokile wanacheza TP Mazembe

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic