November 14, 2020


 KOCHA Mkuu wa Yanga, Cedric Kaze amesema kuwa anaamini wana nafasi ya kufanya vizuri kwenye mechi zao kutokana na hali ya upambanaji wa wachezaji wake ndani ya uwanja.


Kaze ambaye amebeba mikoba ya Zlatko Krmpotic amesepa na tuzo ya kocha bora ndani ya Oktoba akimpoteza Aristica Cioaba wa Azam FC na Francis Baraza wa Biashara United.


Akizungumza na Saleh Jembe, Kaze ambaye mechi yake ya kwanza ya Dar Dabi Novemba 7 alilazimisha sare ya kufungana bao 1-1 Uwanja wa Mkapa alisema kuwa wachezaji wake wanampa matumaini ya kufanya vizuri.


"Ninaona kwamba wachezaji kwenye kila mchezo wamekuwa wakiingia tofauti na kufanya kile ambacho ninakihitaji hilo ni jambo zuri na linaleta matumaini kwangu pamoja na mashabiki pia.


"Kikubwa ambacho ninaweza kusema kwa mashabiki ni kwamba waendelee kujitokeza uwanjani kuipa sapoti timu yao na kuona burudani," .


Kwa mwezi Oktoba pia mchezaji wake Tonombe Mukoko naye amesepa na tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Oktoba akiwapoteza Prince Dube wa Azam FC na Meshack Abraham wa Gwambina FC.

Kesho, Novemba 15 kikosi cha Yanga, kinatarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya African Lyon mchezo utakaochezwa Uwanja wa Azam Complex.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic