November 15, 2020


 EDNA Lema, Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania ya Wanawake chini ya miaka 17 amesema kuwa shukrani kubwa ni kwa Mungu pamoja na wachezaji kujituma bila kusahau sapoti ya mashabiki pamoja na Serikali.


Kwenye mchezo wa fainali ya mashindano ya Cosafa iliyofanyika jana Novemba 14 nchini Afrika Kusini Tanzania iliibuka na ushindi wa jumlajumla baada ya kushinda kwa penalti 4-3 dhidi ya Zambia.


Mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa ulichezwa  Uwanja wa Nelson Mandela, mjini Port Elizabeth, Afrika Kusini,dakika 90 za mwanzo zilikamilika kwa Tanzania kuwa nyuma kwa bao 1-0.

Katika dakika tano za kufidia muda uliopotea katika matukio mbalimbali dakika ya 90+4′ Tanzania ilipata penati baada ya mchezaji wake kufanyiwa madhambi ndani ya boksi. Tanzania ilifanikiwa kusawazisha kupitia penati hiyo iliyopigwa na Koku Kipanga mpaka mwamuzi anapuliza kipenga cha mwisho, Tanzania 1-1 Zambia.


Edna amesema:"Aina gani ya matokeo, aina gani ya ushindi shukrani kwa Mungu ambaye amekuwa pamoja nasi na kutupigania, haikuwa kazi nyepesi ila tumefanikiwa.


"Mashabiki wamekuwa nasi bega kwa bega, Serikali kila mmoja ni ushindi wake huu na Taifa kiujumla,".



5 COMMENTS:

  1. Hongereni sana mabinti zetu. Mmeliletea Taifa letu heshima kubwa. Asanteni sana tena sana

    ReplyDelete
  2. Hongereni sana,timu iandaliwe vizuri kuwa Twiga stars mpya

    ReplyDelete
  3. Kongoree dada zetu kutupa furaha

    ReplyDelete
  4. Timu za wanawake zinajua wanachofanya na niwazalendo was kweli japo hazipewi sapoti kama wanaume(taifa stars)

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic