KOCHA Mkuu wa Yanga, Mrundi, Cedric Kaze, amesema ana imani na mshambuliaji wake, Mghana, Michael Sarpong na hivi karibuni wananchi watamuelewa.
Kauli hiyo aliitoa mara baada ya timu hiyo kufanikiwa kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Biashara juzi kwenye Uwanja wa Karume, Musoma.
Katika mchezo huo, bao la Yanga lilifungwa na Sarpong dakika ya 68.
Akizungumza na Championi Jumatatu, Kaze alisema kuwa mshambuliaji huyo ana uwezo mkubwa wa kufunga mabao, kikubwa alikuwa akitumika vibaya.
Kaze alisema anafurahia kuona nyota huyo akibadilika siku zinavyokwenda. Aliongeza kuwa mshambuliaji huyo akiendelea kupata maelekezo yake huku akizoea mfumo wake, atakuwa tishio.
“Sarpong ni mchezaji mzuri mwenye uwezo mkubwa wa kufunga, ninaamini hapo baadaye atakuwa tushio. Kikubwa ni kumpa muda huku akiendelea kushika maelekezo yangu ili michezo ijayo aongeze hali ya kujiamini. Mashabiki waendelee kumuamini na kumpa sapoti kila anapokuwa uwanjani,” alisema Kaze
0 COMMENTS:
Post a Comment