November 13, 2020


 CLATOUS Chama, nyota wa Klabu ya Simba ameweka bayana mpango wake wa sasa ni kuitumikia timu hiyo na hana mpango wa kuibukia ndani ya Yanga.


Hivi karibuni habari zimekuwa zikieleza kuwa Yanga ipo kwenye mpango wa kuinasa saini ya nyota huyo raia wa Zambia ambaye ana tuzo ya mchezaji bora kwa msimu wa 2019/20 baada ya kutoa jumla ya pasi 10 na kufunga mabao mawili kati ya 78 yalifungwa na Simba.


Kwa sasa Chama mwenye pasi tano na mabao mawili kati ya 22 yaliyofungwa na Simba yupo zake nchini Zambia na timu ya Taifa ambayo jana Novemba 12 ilishinda mabao 2-1 dhidi ya Botswana kwenye mchezo wa kufuzu Afcon.


Chama amesema:"Mimi ni mchezaji wa Simba kwa sasa sina mpango wa kwenda Yanga mjomba, bado nitakuwa ndani ya Simba ikitokea kutakuwa na mabadiliko yoyote kila kitu kitakuwa wazi," .

Desemba 15 dirisha dogo la usajili linatarajiwa kufunguliwa Bongo ambapo jina ambalo limekuwa gumzo kwa sasa ni nyota huyo ambaye wengi hupenda kumuita mwamba wa Lusaka.


Habari kutoka ndani ya Simba zinaeleza kuwa tayari wamemuongezea mkataba wa miaka miwili utakaomfanya abaki ndani ya timu hiyo yenye ngome yake Msimbazi.

5 COMMENTS:

  1. Tetesi nyingi na mpira biashara, waje tuwauzie Kama tulivyowauzia juma Kaseja enzi za manji wakashindwa kumtumia akarejea nyumbani Simba sc, team inayojua biashara yasoka kuliko zote bongo

    ReplyDelete
  2. Gongo wazi waliokuwa wakijitia tamaa na kujigamba CHALI. Sasa upepo utageuka na kaeni tayari

    ReplyDelete
  3. Hahaha huyo ni mchezaji sio shabiki wala mwanachama anaweza kwenda kokote tu muhimu masirahi yake yatekelezwe tu

    ReplyDelete
  4. kwel tanzania akuna team ambayo ita mshnda smb kutoa players

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic