November 10, 2020


RASMI sasa mashabiki wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars wataruhusiwa kushuhudia mtanange kati ya Stars dhidi ya Tunisia ambao ni kwa ajili ya kuwania kufuzu michuano ya Afcon 2021 nchini Cameroon.


Stars ambayo ipo kundi J itaaendelea kusaka ushindi kwenye mchezo dhidi ya Tunisia Novemba 13 ikiwa ugenini ambapo mchezo huo unatarajiwa kuchezwa bila mashabiki kutokana na taarifa kutoka Shirikisho la Soka Afrika (Caf) kutaka iwe hivyo kwa lengo la kuchukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona.


Taarifa iliyotolewa hivi karibuni na Caf wenyewe ilieleza kuwa kikao ambacho walikaa Novemba 4 kupitia video mtandaoni walikubaliana kuendesha mashindano ya Afcon na Ligi ya Mabingwa Afrika pamoja na ile ya Shirikisho bila ya uwepo wa mashabiki.


Leo Novemba 10, taarifa rasmi kutoka Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) imeeleza kuwa wamepewa ruksa ya kuwaruhusu mashabiki kuingia uwanjani kushuhudia mchezo huo wa marudio utakaochezwa Novemba 17, Uwanja wa Mkapa.


Taarifa hiyo imeeleza kuwa kwa sasa TFF inawasiliana na Serikali ili kukidhi matakwa ya Caf ambao wametaka idadi ya watazamaji watakaoingia kwenye mchezo huo kuwa ni asilimia 50 ya uwezo wa Uwanja wa Mkapa.


Kwa sasa Stars ipo Uturuki ambapo imeweka kambi kwa ajili ya maandalizi dhidi ya mchezo dhidi ya Tunisia. 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic