MCHAMBUZI nguli wa masuala ya soka nchini, kwenye kituo cha radio cha TBC Taifa, Mwalimu Alex Kashasha, amefunguka kuwa, hakuwahi kuhisi kama kampuni ya Global Publishers itakuwa na wigo mpana katika nyanja ya habari kama ambavyo amejionea mwenyewe.
Kashasha ameyasema hayo leo Jumanne Novemba 10-2020 alipotembelea ofisi za Global Publishers zIlizopo Sinza Mori Jijini Dar es salaam, inayomiliki magazeti ya Championi, Spoti Xtra, Global TV Online na +255 Global Radio kujionea shughuli mbalimbali za uzalishaji wa habari zinazofanywa na timu ya waandishi, wahariri na watayarishaji wa maudhui tofauti.
Akizungumza kwenye kipindi maalum kilichoruka kwenye spika za Global Radio na kwenda mubashara kwenye ukurasa wa Global Tv Online, Kashasha alisema alikuwa anaifahamu Global kuwa ni kampuni kubwa, lakini hakujua kama ina wigo mpana wa kumiliki vyombo vya habari vya kisasa kama Global TV Onlie, +255 Global Radio na magazeti ya michezo ya Championi, Spoti Xtra na magazeti Pendwa na kueleza kuwa alichokiona baada ya kufanya ziara hiyo kimemshangaza sana.
“Hakika sikuwahi kudhani kama Global ni kubwa kiasi hiki, mimi nilijua ni kitu kidogo kama zilivyo kampuni zingine, kumbe hapa kuna kila aina ya vyombo ambavyo vinatoa habari mbalimbali, kama magazeti, TV na Radio, hakika nimeshangazwa sana.
“Nitoe pongezi kwa uongozi wa kuwaamini vijana, naona vijana wengi hapa hasa wanamichezo huwa tunakutana mara kwa mara viwanjani. Mfano wale mabinti wawili wanaofanya michezo Global TV, (Ester Msophe, Asha Kabuga na Irene Kilango), ni wachapakazi sana, mara nyingi huwa wananifuata na kufanya nao kazi. Hongereni sana,” alisema.
Kashasha ambaye amejizolea umaarufu mkubwa kwa miaka ya hivi karibuni hasa kutokana na aina yake ya uchambuzi na mpangilio wa kuyaelezea matukio ya uwanjani kwa lugha ya Kiingereza, amekuwa kivutio kwa watu wengi sana.
Kazungumza vitu mbalimbali kwenye mahojiano hayo ambayo yapo tayari Global TV Online, unaweza kwenda Youtube na kuyasikiliza. Huko pia kalitaja bao lake bora alilowahi kulishuhudia, mchezaji anayemkubali na kazungumza juu ya Clatous Choma kuhusu uvumi wa kwenda Yanga
0 COMMENTS:
Post a Comment