HASSAN Mwakinyo, bondia Mtanzania amesema kuwa alijipanga kuibuka na ushindi mbele ya mpinzani wake Jose Carlos Pazi wa Argentina jambo lililompa ushindi.
Bondia Mwakinyo usiku wa kuamika leo amefanikiwa kuetetea mkanda wake wa WBF Intercontinental Super Welterweight.
Mwakinyo amemchapa Paz wa Argentina kwa TKO raundi ya nne kwenye Ukumbi wa Next Door Arena.
"Nilikuwa nimejipanga kushinda na ninafurahi kushinda katika hili huu ni ushindi wa Tanzania kiujumla, mashabiki pamoja na Serikali ambayo inanipa sapoti," amesema.
Mwakinyo kongore watanzania vicheko tu
ReplyDeleteHongera sana kaka umepeperusha vizuri bendera ya taifa.Ila nakuomba usikubali kupigana pambano lisilo la mkanda na Twaha Kiduku,mapando kama haya yatakuvunjia heshima.Kumbuka yaliyotokea kwa Cheka alipopigana mapambano yasiokuwa na maana,nyota zake kimataifa ziliposhuka.Zingatika kauli za mheshimiwa Kikwete aliposema kumpiga kijembe cheka,nakuu Mwenzetu ulishafika level nzuri kimataifa,haya mapanbano mengine yasiokuwa ya maana yanakuvunjia heshima,ww sio wa level hiyo tena huko ulishatoka,ww wa kujipambanua kimataifa zaidi.
ReplyDeleteUliteseka sana kuijenga hiyo Cv usiibomoe kirahisi tena kwa faida ya wachache.
ReplyDelete